Monday , 6 May 2024
Home Habari Mchanganyiko Washindi saba safarini Dubai NMB MastaBata ‘Kote Kote’
Habari Mchanganyiko

Washindi saba safarini Dubai NMB MastaBata ‘Kote Kote’

Spread the love

KAMPENI ya kuhamasisha matumizi ya Mastercard na QR Code ‘Lipa Mkononi’ iitwayo NMB MastaBata ‘Kote Kote’, imefikia ukomo jana Jumanne tarehe 7 Februari 2023 kwa wateja saba na wenza wao kujishindia safari ya Dubai kwa siku nne inayogharamiwa kila kitu na NMB, kuhitimisha miezi mitatu iliyotoa zawadi mbalimbali zenye thamani ya zaidi ya Sh350 milioni. Anaripoti Mwandishi Wetu…(endelea).

NMB MastaBata ‘Kote Kote’ ni msimu wa nne wa kampeni hiyo uliozinduliwa Oktoba 28, 2022a, ikichagiza matumizi yasiyohusisha pesa taslimu ‘cashless,’ ambako kulikuwa na zawadi za kila wiki, mwezi na ‘grand finale’ hiyo iliyohusisha pia wafanyakazi wawili wa benki hiyo kinara nchini.

Afisa Mkuu wa Wateja Binafsi na Biashara wa Benki ya NMB, Filbert Mponzi (wa pili kushoto) na Balozi wa Kampeni ya MastaBata ‘Kote Kote’, Millard Ayo (wa pili kulia), wakibonyeza kwa pamoja kitufe cha kompyuta wakati wa droo ya kutafuta washindi saba wa ‘Grand Finale’ ya kampeni hiyo iliyofanyika jijini Dar es Salaam jana. Kushoto ni Mkuu wa Kitengo cha Kadi wa benki hiyo, Philbert Casmir na kulia ni Msimamizi kutoka Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania (GBT), Upendo Mfuru.

Katika droo ya fainali iliyosimamiwa na Pendo Mfuru kutoka Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania (GBT), walioibuka washindi wa safari ya Dubai ni: Upendo Yohana Msanjila (Dar), Edwin Sett Mwakabage (Kilimanjaro) na Benigna Xaveria Hyera (Dar).

Washindi wengine wa droo hiyo iliyochezeshwa na Balozi wa NMB MastaBata ‘Kote Kote’, Millard Ayo, ni pamoja na Nazia Abdulsatar Lakha (Dar), John Wayne Lubisha (Dodoma) na Chintan Chandrakant Kamania (Dar).

Kabla ya ‘grand finale’ hiyo, jumla ya washindi 750 walishinda pesa kiasi cha Sh. 100,000 kila mmoja, wengine 98 wakizawadiwa Sh. Mil. 1 kila  mmoja, huku washindi 12 wakitwaa bodaboda moja moja zenye thamani ya Sh. Mil. 3 kila moja. Aisha, washindi wengine wanne walijishindia safari ya Zanzibar kuhudhuria Tamasha la NMB Full Moon Party.

Awali, kabla ya droo ya fainali, Afisa Mkuu wa Biashara na Wateja Binafsi wa NMB, Filbert Mponzi, alibainisha kuwa kampeni hiyo imekuwa ya mafanikio makubwa kwa kufanikiwa kubadili tamaduni za matumizi ya kadi na QR Code, na kuwa matokeo ya faida kubwa ya Sh. Bilioni 429 baada ya kodi kwa mwaka 2022, yametokana na promosheni kama hizo.

“Ni kampeni chanya iliyoongeza matumizi ya kadi, ambayo ni salama, rahisi na nafuu zaidi, huku ikitoa mchango katika rekodi yetu ya faida baada ya kodi. Wito wetu Kwa Watanzania, wafungue akaunti na kufanya matumizi yasiyohusisha pesa taslimu, ili kujiweka katika nafasi za kunufaika na kampeni zaidi zijazo na promosheni nyinginezo,” alibainisha Mponzi.

Mapema kabla ya droo hiyo, Philbert Casmir ambaye ni Mkuu wa Kitengo cha Kadi NMB, alisema benki yake inajivunia mafanikio yaliyotokana na MastaBata ‘Kote Kote’, kampeni endelevu iliyokuwa na malengo matatu ya kuzawadia washindi, kuhamasisha matumizi salama na nafuu ya kadi, pamoja na kurejesha kwa Jamii sehemu ya faida yao kwa mwaka uliopita.

Naye Ofisa wa Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania (GBT), Pendo Mfuru, aliipongeza NMB kwa aina ya ushirikiano iliyonao kwa taasisi yake iliyo na mamlaka ya kusimamia michezo hiyo nchini, ikiwamo kuratibu, kuendesha na kuzawadia washindi kwa kuzingatia vigezo na masharti ya GBT, huku akiwapongeza zaidi ya washindi 870 walioibuka na zawadi mbalimbali za kampeni hiyo.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Tanzania  yasisitiza kuwa Kituo Kikuu cha Uchimbaji Madini Afrika

Spread the loveTanzania imeendelea kusisitiza adhma yake ya kuwa kituo kikuu cha...

Habari MchanganyikoTangulizi

Kimbunga Hidaya chatikisa Mafia

Spread the loveWAKATI hali ya upepo mkali ikiendelea kushuhudiwa katika baadhi ya...

Habari MchanganyikoTangulizi

Usafiri baharini wasitishwa kukwepa athari za kimbunga Hidaya

Spread the loveUSAFIRI wa baharini umesimamishwa kwa muda ili kukwepa athari za...

Habari Mchanganyiko

RPC Dodoma akabidhiwa bunduki mbili za wahalifu

Spread the love  Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa ya Kulevya...

error: Content is protected !!