IDADI ya vifo vilivyotokana na tetemeko la ardhi lililotokea Jumatatu wiki hii nchini Syria na Uturuki vimefikia 9,000. Inaripoti Mitandao ya Kijamii … (endelea).
Timu za waokoaji katika nchi hizo nchi ziliendelea kuwatafuta manusura waliofukiwa kwenye vifusi vya majengo yaliyoangushwa na matetemeko makubwa ya ardhi yaliyozikumba nchi hizo.
Zaidi ya mitetemeko 20 kati ya hiyo ilikuwa na kipimo cha 4.0 au zaidi, na kutikisa eneo lililo kwenye mpaka kati ya nchi hizo mbili.
Mkurugenzi mkuu wa Shirika la Afya Duniani (WHO), Tedros Ghebreyesus ameelezea kuwa pamoja na wananchi wa Uturuki na Syria katika kipindi hiki cha huzuni mkubwa.
Amesema idadi ya vifo haizingatii huzuni na hasara zinazopitia familia hivi sasa ambazo zimepoteza baba, mama, binti, mtoto chini ya vifusi, au ambazo hazijui kama wapendwa wao wako hai au wamekufa.
Akizungumza kwenye mkutano wa WHO mjini Geneva, Tedros amesema shirika hilo linatuma ndege za kukodi na vifaa vya matibabu kwa nchi zote mbili na kwamba litafanya kazi kuwasaidia watakapopata afueni na kujenga upya.
Leave a comment