Tuesday , 7 May 2024
Home Habari Mchanganyiko Serikali: Tanzania haina maambukizi mapya ya ukoma
Habari Mchanganyiko

Serikali: Tanzania haina maambukizi mapya ya ukoma

Spread the love

NAIBU Waziri wa Afya Dk. Godwin Mollel amesema kwa sasa Tanzania imepiga hatua katika kupambana na ugonjwa huo na wagonjwa wanaopatikana siyo maambukizi mapya bali ni wagonjwa zamani. Anaripoti Danson Kaijage, Dodoma (endelea).

Dk. Mollel ametoa kauli hiyo jana tarehe 29 Januari 2023 wakati akizungumzia kilele cha siku ya ukoma duniani ambapo pamoja na mambo mengine amesema wagonjwa wapya wa ukoma waliogundulika nchini imepungua mwaka hadi mwaka, katika miongo miwili iliyopita ambapo dunia iliongeza kasi ya kupambana na ugonjwa huo.

“Nchi yetu imeweza kuwagundua na kuwatibu wagonjwa wapya wa  ukoma zadi ya 122,000 na kwa mwaka 2021 walikuwepo wagonjwa wapy 1,613.

“Tanzania tayari imefikia hatua ya awali ya kiwango cha kimataifa cha utokomezaji wa ukoma na kuwa chini ya mgonjwa mmoja kati ya watu 10,000 kwa mto mmoja kwa idadi hiyo katika nchi au katika sehemu husika.

“Hatua zinazofuata ni kutokuwa na mtoto anayeugua ukoma nchini kwa miaka mitatu, mitano na hatimaye 10 mfululizo, kwa mwaka 2021 kwa watoto waliogundulika kuugua ukoma ilifika 41 na hivyo kuonesha wazi ya kuwa mnyororo wa maambukizi bado upo na bado tuna jukumu kubwa la kufanya kukomesha kuenea kwa ugonjwa huo na kwa sasa wagonjwa wengi wanaogundulika ni wale wa zamani” ameeleza  Dk. Mollel.

Hata hivyo, Dk. Mollel alitaja mikoa mbayo imekuwa na wagonjwa wengi wa ukoma kuwa ni Morogoro, Lindi, Dar es Salaam, Pwani, Mtwara, Tanga, Katavi, Dodoma, Geita, Shinyanga, Tabora na Rukwa.

Pamoja na mambo mengine Dk. Mollel amekabidhi gari la kubebea wagonjwa katika hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Dodoma kama sehemu ya kuwezesha kurahisisha utendaji kazi.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Mahakama yatoa uamuzi zuio dhidi ya Club House

Spread the loveMAHAKAMA Kuu ya Tanzania, Masjala Kuu jijini Dar es Salaam,...

Habari Mchanganyiko

GGML, OSHA yawanoa bodaboda 200 Arusha

Spread the loveZAIDI ya madereva bodaboda 200 wa jiji la Arusha wamepatiwa...

BiasharaHabari Mchanganyiko

Serikali kuwakopesha wajasiriamali 18.5bn/- kupitia NMB

Spread the loveSerikali imetenga kiasi cha Sh 18.5 bilioni kwa ajili ya...

AfyaHabari Mchanganyiko

Huduma za kibingwa zazinduliwa katika hospitali za halmashauri 184

Spread the loveSERIKALI imezindua huduma za matibabu za kibingwa katika hospitali 184...

error: Content is protected !!