Thursday , 25 April 2024
Home Kitengo Maisha Afya Ma-RMO, DMO watakiwa kujitafakari ubadhirifu hospitali za mikoa, wilaya
Afya

Ma-RMO, DMO watakiwa kujitafakari ubadhirifu hospitali za mikoa, wilaya

Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto nchini Tanzania, Dk. Godwin Mollel
Spread the love

 

NAIBU Waziri wa Afya, Dk. Godwin Mollel, amewataka waganga wakuu wa Hospitali za Mikoa na Wilaya ambao unafanyika ubadhirifu katika vituo vyao vya kazi lakini hawajiu namna unavyotokea ni vyema wakaanza kujitafakari upya. Anaripoti Danson Kaijage, Dodoma … (endelea).

Dk. Mollel ametoa rai hiyo jana tarehe 29 Jauari mwaka 2023 wakati akizungumza na waandishi wa habari pamoja na baadhi ya watumishi wa Wizara hiyo wakati alipokuwa akisoma tamko kwa niaba ya Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu juu ya kuelekea kilele cha siku ya Ukoma Duniani ambayo ufanywa kila mwisho wa wiki ya Mwezi wa Januari.

Dk. Mollel amesema kuwa pamoja na serikali ya awamu ya Sita ambayo inaongozwa na Rais Dk. Samia Suluhu Hassan, kuwekeza zaidi katika sekta ya afya kwa kuongeza majengo, vifaaa vya kisasa lakini bado kuna changamoto kubwa kwa uboreshaji wa huduma ya afya kwa watendaji.

“Inasikitisha kumkuta mganga mkuu wa Mkoa au wilaya au mkuu wa kituo wanapokwenda viongozi wa juu kutoka serikalini au wizarani na kukuta madudu, wakiwa wanashangaa na mganga mkuu wa Mkoa au mganga mkuu wa Wilaya naye anashangaa.

“Jambo hilo haliwezi kuvumiliwa na kama litaendelea kuwa hivyo itakuwa butua nikubutue kwani kila mmoja anatakiwa kucheza mpira kwa namba yake na si vinginevyo” amesema Dk.Mollel.

Pamoja na mambo mengine ambayo amesisitiza yafanyike ni pamoja na kuwaomba waganga wakuu wa mikoa na waganga wakuu wa wilaya wanapopokea dawa kutoka Bohari kuu ya madawa (MSD) kuwashirikisha wakuu wa wilaya na wakuu wa mikoa.
“Hao ni wenyeviti wa kamati ya ulinzi na usalama na njia hiyo inaweza kuwa sehemu ya kuboresha ubora wa huduma ya afya.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Afya

Mloganzila yajipanga kupandikizaji wa ini

Spread the love  HOSPITALI ya Taifa Muhimbili-Mloganzila imesema kutokana na uwekezaji uliofanywa...

AfyaHabari za Siasa

Serikali yasaka watumishi afya ngazi ya jamii 8,900

Spread the loveSERIKALI imeanza utekelezaji wa mpango jumuishi wa wahudumu wa afya...

AfyaHabari za SiasaTangulizi

Bima ya afya kwa wote kuanza Aprili, wajane kicheko

Spread the loveSHERIA ya Bima ya Afya kwa Wote, inatarajiwa kuanza kutumika...

AfyaHabari Mchanganyiko

Marekani kuipa Tanzania bilioni 980 kudhibiti VVU, UKIMWI

Spread the loveSERIKALI ya Tanzania inatarajiwa kupewa msaada wa fedha kiasi cha...

error: Content is protected !!