Friday , 29 March 2024
Home Habari Mchanganyiko Bashe: Serikali haitamzuia mkulima kuuza mazao kwa bei anayotaka
Habari Mchanganyiko

Bashe: Serikali haitamzuia mkulima kuuza mazao kwa bei anayotaka

Spread the love

WAZIRI wa Kilimo, Hussein Bashe, amesema Serikali haitazuia wakulima kuuza mazao yao kwa bei wanayotaka kwa kuwa kitendo hicho kinaminya maslahi yao. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam…(endelea).

Bashe ametoa kauli hiyo leo tarehe 30 Januari 2023, Ikulu jijini Dar es Salaam, baada ya waandishi wa habari kuhoji kwa nini Serikali isizuie uuzaji holela wa mazao unaosababisha mfumuko wa bei ya vyakula nchini.

“Tutamruhusu mtu yeyote kutoka popote kununua mazao ya mkulima kama ilivyo biashara nyingine, kwanza niweke sawa kwamba mazao ya wakulima ni mali yao wana haki ya kuyauza popote,” amesema Bashe.

Katika hatua nyingine, Bashe amesema ili kuondoa changamoto ya uuzaji holela wa mazao, Serikali imeanzisha utaratibu wa kuweka vituo vya uuzaji mazao maeneo ambayo wakulima wapo.

Kuhusu mfumuko wa bei ya vyakula, Bashe amesema Serikali itaendelea kununua mazao kutoka kwa wakulima kisha kuyasambaza kwa wananchi kwa bei nafuu.

“Rais amezindua ghala kubwa la NFRA mkoani Manyara, sasa hivi uwezo wetu wa kuhifadhi umeongezeka kutoka tani 200,000 hadi 500,000. Hivyo tutayahifadhi na hatutamzuia mkulima kuuza mazao yake popote sababu siyo haki,” amesema Bashe.

Katika hatua nyingine, Bashe amesema Serikali imeamua kufanya upembuzi yakinifu katika mabonde yote nchini kwa ajili ya kuimarisha kilimo cha umwagiliaji ili kuongeza uzalishaji mazao kwa lengo la kupunguza mfumuko wa bei, ambapo kwa kuanzia imetenga Sh. 36 bilioni kwa ajili ya kufanya upembuzi katika mabonde 22.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Puma Energy Tz: Watanzania tudumishe amani kuvutia uwekezaji

Spread the loveKAMPUNI ya Mafuta ya Puma Tanzania imewakutanisha wadau mbalimbali katika...

Habari Mchanganyiko

DAWASA waanza utekelezaji agizo la Samia

Spread the loveMamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam...

Habari MchanganyikoKimataifa

Zuma akataliwa kugombea urais

Spread the loveTUME Huru ya Uchaguzi Afrika Kusini (IEC) imemwondoa rais wa...

Habari Mchanganyiko

Mtandao watetezi wa haki za mazingira Tanzania waundwa

Spread the loveMTANDAO wa watetezi wa haki za mazingira nchini Tanzania, umeundwa...

error: Content is protected !!