Tuesday , 7 May 2024
Home Kitengo Maisha Afya Chanzo mzozo wa muuguzi, mtaalamu wa maabara Uyui chabainika
Afya

Chanzo mzozo wa muuguzi, mtaalamu wa maabara Uyui chabainika

Spread the love

 

CHAMA cha Wauguzi Tanzania (TANNA) kimetoa taarifa ya uchunguzi wa tukio la watumishi wa kada ya Afya wa Zahanati ya Ishihimulwa wilaya ya Uyui mkoani Tabora waliokuwa wanazozana kuhusu kutumia vipimo vya malaria RDT ambavyo mmoja wao alidai vimeisha muda wake wa matumizi na kubainisha kuwa kulikuwa na mgogoro binafsi baina yao. Anaripoti Mwandishi Wetu, Tabora … (endelea).

Taarifa ya uchunguzi huo imetolewa leo Alhamisi tarehe 12 Januari 2023 na Ofisi ya Uenezi na Habari ya chama hicho ikiwa ni siku chache tangu kutokea kwa tukio hilo.

Itakumbukwa kuwa hivi karibuni katika mitandao ya kijamii ilisambaa video ikimwonesha mtaalamu wa maabara James Chuchu akizozana na muuguzi Rose Shirima kuhusu matumizi ya vipimo vya malaria ambavyo vilidaiwa kuwa vimeisha muda wake.

Katika video hiyo muuguzi alisisitiza mtaalamu huyo atumie vipimo hivyo kwa wajawazito huku akimtupia maneno ya kejeli kuwa ana kiherehere cha kutaka kuwa mfanyakazi bora.

Hata hivyo taarifa ya TANNA imebainisha kuwa mtaalamu wa maabara alimtusi muuguzi kabla ya kuanza kurekodi kitendo ambacho kilimfanya muuguzi atoe majibu yasiyo na staha.

Chama kimebaini uwepo wa mgogoro wa muda mrefu baina ya hao watumishai na hata hivyo kabla ya kuanza kurekodi video kulikuwa na lugha ya matuzi kutoka kwa mteknolojia wa maabara kwenda kwa muuguzi hali iliyomfanya muuguzi kufadhaika na kujikuta akimjibu kwa lugha isiyo na staha,” imeeleza taarifa hiyo.

Katika hatua nyingine chama hicho kimewatoa hofu wananchi wanaopata huduma kwenye Zahanati hiyo kuwa hakuna vitendanishi vyovyote vilivyoisha muda wake ambavyo vilikuwa vinatumika katika kituo hicho.

Chama hicho kimewakumbusha watumishi wa Afya kujenga utamaduni wa kuwa na vikao vya ndani na kuanzisha kamati za maadili kuanzia ngazi ya vituo ili kusaidia kutatua matatizo ya kitaaluma kwa wakati.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

AfyaHabari Mchanganyiko

Huduma za kibingwa zazinduliwa katika hospitali za halmashauri 184

Spread the loveSERIKALI imezindua huduma za matibabu za kibingwa katika hospitali 184...

AfyaHabari Mchanganyiko

200 wapimwa afya na GGML katika maonesho ya OSHA

Spread the loveZAIDI ya watu 200 jijini Arusha wamejitokeza kupimwa afya na...

AfyaHabari za Siasa

Dk. Biteko aagiza utoaji huduma saratani usiwe wa kibaguzi

Spread the loveNaibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto Biteko...

AfyaHabari Mchanganyiko

Songwe katika mikakati ya elimu ya lishe kudhibiti udumavu

Spread the love  SERIKALI mkoani Songwe imejipanga kuendelea kutoa elimu ya lishe...

error: Content is protected !!