MAHAKAMA Kuu Zanzibar Masjala ya Tunguu imesema kuwa Chama cha Wananchi CUF hakina ushahidi wa kutosha wa kuithibitishia mahakama hiyo kuwa majengo ya Chama cha ACT-Wazalendo ni yao. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).
Hukumu hiyo imetolewa Jumatano tarehe 11 Janauri, 2023 na Jaji George Kazi baada ya kusikiliza kwa miaka mitatu shauri hilo namba 16 ya Mwaka 2019 kwa miaka mitatu .
Shauri hilo lilifunguliwa na Bodi ya wanadhamini ya Chama cha Wananchi CUF, wakiwalalamikia wanachama 19 wa ACT akiwemo Kiongozi wa Chama hicho Zitto Kabwe.
Walalamikiwa wengine kwenye shauri hilo ni pamoja na Salim Bimani, Joran Bashange, Ismail Jussa, Nassoro Mazrui, Thubeit Khamis Faki, Saleh Nassor Juma, Awadh Ali Said, Ali Abdallah, Zahra Ali Hamad, Raisa Abdallah Mussa, Fat’hiya Zahran, Said Ali Mbarouk, Riziki Omar Juma, Mohamed Juma Khatib, Tahir Awezi Mohamed. Khatib Hamad Shehe, Ali Abeid, Juma Abdulla Khatib, na Chama cha ACT Wazalendo.
CUF ililalamika kuporwa majengo ya Chama hicho pamoja na lile la Vuga, Mtendeni Ofisi ya Kilima Hewa, Mfenesini, Ofisi ya CUF ya Wilaya ya Micheweni iliyokuwepo Majenzini, Ofisi ya Koani iliyokuwa kwenye sheha ya Changaweni, Chumani, Nungwi Kaskazini ‘A’, Mkototoni, Ofisi ya Chakechake, sambamba na matawi kadhaa huku visiwani Zanzibar.
Jaji Kazi kwenye hukumu yake ameeleza kuwa CUF haikuwa na nyaraka zitakazoweza kuithibitishia mahakama hiyo kuwa majengo hayo ni halali yao.
Leave a comment