Tuesday , 7 May 2024
Home Habari Mchanganyiko JUKATA yataka ratiba mchakato marekebisho ya sheria, katiba mpya
Habari Mchanganyiko

JUKATA yataka ratiba mchakato marekebisho ya sheria, katiba mpya

Spread the love

JUKWAA la Katiba Tanzania (JUKATA), limeiomba Serikali kutoa ratiba ya utekelezaji wa marekebisho ya Sheria na namna ya kukwamua mchakato wa upatikanaji katiba mpya, ili kuruhusu ushiriki mpana wa wadau na wananchi. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam…(endelea).

Wito huo umetolewa leo Jumatano, tarehe 4 Januari 2022 na Mkurugenzi Mtendaji na Katibu wa Bodi wa JUKATA, Bob Wangwe, siku Moja baada ya Rais Samia Suluhu Hassan, kusema Serikali yake Iko tayari kukwamu mchakato wa marekebisho ya katiba uliokwama 2014.

“JUKATA tunaisihi Serikali kutoa ratiba ya utekelezwaji wa marekebisho ya Sheria na namna ya kukwamua mchakato wa katiba moya Ili kuruhusu ushiriki Mpana wa wadau na wananchi kwenye michakato hiyo,” imesema taarifa ya Wangwe.

Aidha, Wangwe amesema JUKATA iko tayari kutoa ushirikiano na usaidizi wa kitaalamu katika kuhakikisha utekelezaji wa michakato hiyo inafanikiwa kwa lengo la kujenga demokrasia.

Katika hatua nyingine, JUKATA imempongeza Rais Samia kwa kuondoa zuio la  mikutano ya hadhara, kufanya marekebisho ya Sheria na utayari wake wa kukwamua mchakato wa katiba.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Mahakama yatoa uamuzi zuio dhidi ya Club House

Spread the loveMAHAKAMA Kuu ya Tanzania, Masjala Kuu jijini Dar es Salaam,...

Habari Mchanganyiko

GGML, OSHA yawanoa bodaboda 200 Arusha

Spread the loveZAIDI ya madereva bodaboda 200 wa jiji la Arusha wamepatiwa...

BiasharaHabari Mchanganyiko

Serikali kuwakopesha wajasiriamali 18.5bn/- kupitia NMB

Spread the loveSerikali imetenga kiasi cha Sh 18.5 bilioni kwa ajili ya...

AfyaHabari Mchanganyiko

Huduma za kibingwa zazinduliwa katika hospitali za halmashauri 184

Spread the loveSERIKALI imezindua huduma za matibabu za kibingwa katika hospitali 184...

error: Content is protected !!