Monday , 13 May 2024
Home Habari Mchanganyiko Ataka waliochoma vifaranga washughulikiwe
Habari Mchanganyiko

Ataka waliochoma vifaranga washughulikiwe

Mratibu wa THRDC, Onesmo Olengurumwa
Spread the love

 

MCHAMBUZI wa masuala ya mifugo, Onesmo Olengurumwa, ameiomba Serikali iwachukulie hatua watu waliochoma vifaranga kutokana na kukosa soko, akisema ni kinyume cha Sheria ya Usalama na Ustawi wa Wanyama ya mwaka 2008. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Olengurumwa ametoa wito huo leo Ijumaa, tarehe 23 Desemba 2022, ikiwa zimepita siku kadhaa tangu shamba la kuku la Kibo, mkoani Kilimanjaro, kuteketeza vifaranga vilivyokosa soko jijini Dar es Salaam.

“Yeyote yule anayefuga wanyama anapaswa kuzingatia haki za wanyama ambazo hazitofautiani na haki za binadamu, mfano kitendo hiki cha kuchoma vifaranga ni kinyume na haki za wanyama na uhuru dhidi ya ukatili na maumivu makali. Sheria hii imekataza mazingira yoyote yanayotweza utu wa mnyama na kumwekea maumivu makali,” amesema Olengurumwa.

Olengurumwa amesema, vifaranga hivyo vilipaswa kutolewa bure kwa wafugaji kama vilikuwa havina magonjwa ya mlipuko.

“Baraza la ustawi wa wanyama au wakaguzi wa wanyama wa eneo hilo wawaite wajieleze ili pia iwe elimu kwa watanzania wengine wanaofuga. Sheria pia inataka kila wilaya kuwe na mkaguzi na mlinzi wa usalama wa wanyama, kama mpo teteeni wanyama,” amesema Olengurumwa.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Msukuma aibana Serikali ujenzi nyumba za watumishi Geita DC

Spread the loveMBUNGE wa Geita, Joseph Msukuma (CCM) ameishauri Serikali kutenga bajeti...

AfyaHabari MchanganyikoHabari za Siasa

NBC yazindua kadi uanachama msalaba mwekundu

Spread the loveNaibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto Biteko...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Dk. Biteko: Serikali itaendelea kushirikiana na Red Cross

Spread the loveNaibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto Biteko...

Habari MchanganyikoHabari za SiasaTangulizi

Dk.Mpango aagiza trafki kuvaa makoti ya kamera kudhibiti rushwa

Spread the loveMakamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk....

error: Content is protected !!