Sunday , 28 April 2024
Home Habari Mchanganyiko Wamiliki runinga za mitandaoni zinazotoa taarifa za uongo mbaroni
Habari Mchanganyiko

Wamiliki runinga za mitandaoni zinazotoa taarifa za uongo mbaroni

Kamanda Polisi wa Kanda ya Dar es Salaam, Jumanne Murilo
Spread the love

 

JESHI la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam kwa kushirikiana na timu maalum ya kuzuia na kupambana na makosa ya mtandao limewakamata watuhumiwa 11 wa makosa ya kimtandao kufuatia ufuatiliaji mkali uliofanyw ana jeshi hilo. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Akizungumza na waandishi wa habari Jijini Dar es Salaam Kamanda Kanda Maalum ya Polisi Dar es Salaam, ACP Muliro Mulilo, amesema Jeshi la Polisi na timu hiyo, limemkamata Alex Magoti (26) Mkazi wa Tabora Mjini na wenzake wanane kwa tuhuma za kumiliki luninga za mtandaoni na akaunti za mitandao ya kijamii ambazo zimekuwa zikitumika kusambaza taarifa za uongo au uzushi kuhusu, Rais Dk. Samia Suluhu Hassan na viongozi wengine wakuu wa Serikali.

Aidha amesema watuhuhumiwa hao wamekuwa wakiweka taarifa za uzushi, uongo na upotoshaji kwenye luninga za mtandaoni zinazotambulika kwa majina ya BSUN Online TV, GATTU Online TV, TAMUTAMU online TV, KILIMANJARO online TV na nyinginezo.

“Mfano wa taarifa hizo ni kama; Rais Samia akosoa vikali utawala wa Rais JPM, aanika ukatili aliofanya (haukubaliki hata kidogo)” “IMEVUJA VIDEO, MBOWE APEWA SHAVU…!”, “DENI LA TAIFA LAIBUA MAZITO MWIGULU KUTUMBULIWA…!”, “GHAFLA MKE WA MAGUFULI AFA…!”, “ITAKUTOA MACHOZI UKWELI WOTE KIFO CHA MAGUFULI,” amesema Muliro.

Sambamba na hayo Jeshi la Polisi limemkamata, Joseph Mzava (19) mkazi wa Kinondoni Dar es Salaam, mwanafunzi wa mwaka wa kwanza Chuo cha Biachara Dar es Salaam (CBE), kwa tuhuma za kujinasabisha kuwa yeye ni Rais Mstaafu Jakaya Kikwete na kufanikiwa kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu kupitia mtandao kwa kutumia laini za simu zenye usajili usio na majina yake.

Jeshi la Polisi pia limemkamata LI Naiyong (48) raia wa China, ambaye anatuhumiwa kujihusisha na shughuli za kuingilia mfumo wa mawasiliano kinyume na taratibu za nchi, na kuisababishia Serikali hasara ya kiasi cha Sh. 221 milioni.

“Mtuhumiwa huyo amekuwa akituma vifaa visivyo rasmi kuwaunganisha watu kwa simu kufanya mawasiliano nje ya nchi kinyume na sheria za mmlaka ya mawasiliano Tanzania (TCRA),” amesema Kamanda Muliro.

Hata hivyo amesema watuhumiwa hao wamekutwa wakiwa na vifaa mbalimbali ambavyo wanavitumia kufanya uhalifu huo, ambavyo ni Simu za mkononi 23, Laini za Simu 437 za makampuni mbalimbali ya huduma za simu zenye usajili wa watu tofauti tofauti, Kompyuta Mpakato 6, Sim Box 5, Routers 3 na Power Bank 1

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

NBC yapata tuzo ya mwezeshaji bora wa mikopo serikali Afrika

Spread the loveBenki ya NBC imepata tuzo ya Mwezeshaji Bora wa Pamoja...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Biteko aipongeza GGML kudhibiti vifo, majeruhi mahali pa kazi

Spread the loveNAIBU Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto Biteko...

Habari Mchanganyiko

Wami Ruvu hawana deni la Rais Samia katika kutunza vyanzo vya maji

Spread the love  BODI ya Maji Bonde la Wami Ruvu, imeendelea kuchua...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Mavunde aibana kampuni kutimiza masharti ya mkataba

Spread the loveWaziri wa Madini, Anthony Mavunde ameitaka Kampuni ya Xin Tai...

error: Content is protected !!