Saturday , 11 May 2024
Home Habari Mchanganyiko Mkazi Dodoma akabidhiwa pikipiki ya Mastabata
Habari Mchanganyiko

Mkazi Dodoma akabidhiwa pikipiki ya Mastabata

Spread the love

MKAZI wa Kizota jijini Dodoma, Salum Jumanne Rajabu jana Alhamisi Desemba 15, 2022 alikabidhiwa pikipiki yake baada ya kushinda katika shindano la MastaBata Kote kote linaloendeshwa na Benki ya NMB. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dodoma…(endelea).

Rajab alikabidhiwa pikipiki hiyo na Meneja wa NMB Tawi la Kambarage Jijini Dodoma Emiliana Wilson ambaye alisema mshindi huyo alipatikana katika shindano la Mastabata Kote Kote lililoendeshwa wiki iliyopita.

Meneja wa NMB Tawi la Kambarage,Emiliana Wilson (kushoto) akimkabidhi kadi ya pikipiki msindi wa droo ya mastaBata kotekote ,Salumu Jumanne (katikati) ambaye ni ,alishinda kwenye droo ya nne iliyochezshwa wiki iliyopita , makabidhiano hayo ya pikipiki hiyo yalifanyika Jijini Dodoma jana ,kulia ni Meneja mwandamizi wa fedha kitengo cha kadi benki ya NMB ,Erick Emmanuel.

Akikabidhi pikipiki hiyo, Emiliana alisema ushindi katika shindano hilo siyo tatizo gumu bali siri yake ni kutumia MasterCard ya Benki ya NMB katika kufanya miamala.

Meneja alisema hadi jana shindano hilo ambalo linakwenda awamu ya tano, walishatoa zaidi ya Sh100 milioni kwa washindi 300 lakini hivi karibu wametoa pikipiki 2 na fedha kwa washindi.

“Shindano letu halibagui, tunashindanisha Wateja wetu wote wanaotumia MasterCard, wapo wanaoshinda Sh 100,000, wanaoshinda pikipiki na Wengine mwanzoni mwa Mwaka watashinda safari ya Dubai ambayo kila mshindi atakwenda na mwenza wake na kukaa huko kwa siku nne,” alisema Emiliana.

Jana, Meneja huyo alichezesha shindano hilo kutokea Dodoma ambapo mshindi wa pikipiki alipatikana Shamsanga Samu kutoka Kimara huku Sia Rajabu kutoka Msasani akiwa miongoni mwa washindi 75 waliojishindia Sh 100,000.

Meneja wa NMB Tawi la Kambarage, Emiliana Wilson (katikati) akibonyeza kitufe cha kompyuta kuashiria kuzindua droo ya tano ya mastercard KOTEKOTE iliyochezeshwa Tawi la Kambarage Jijini Dodoma. Kushoto ni Meneja mwandamizi wa fedha kitengo cha kadi benki ya NMB, Erick Emmanuel na kulia ni Mkaguzi kutoka Bodi ya michezo ya Bahati nasibu, Goodluck Msomigulu.

Meneja Mwandamizi Idara ya Fedha na uwezeshaji katika biashara za kadi kwa Benki ya NMB Erick Emmanuel alisema wataendelea kumwaga noti kwa washindi hivyo wajitokeze kushiriki.

Emanuel alisema awamu zilizotangulia zimekuwa na mafanikio makubwa ambapo washindi wametoka kila kona ya nchi hivyo mafanikio hayo yamepelekea kuanza kwa msimu wa tano ambao utaratibu wake ni kuchezesha shindano hilo kupitia matawi yake yote kwa zamu.

Akizungumza mara baada ya kukabidhi wa pikipiki yake, Salum Rajabu alisema hakutegemea kama angeshinda kwani hakuamini kama anafanya mashindano.

Rajabu alisema ni utaratibu wake kutumia Master Card kwa ajili ya kufanya miamala na kulipia huduma mbalimbali kupitia kadi yake.

“Kwamba ningeibuka mshindi hiyo sikujua, lakini pia sikujua kama nilikuwa nashindana ila napenda kutumia mfumo huu kwa sababu ni rahisi na salama zaidi, hivyo itakuwa jambo jema niseme kuwa tuendelee kutumia mafumo huu,” alisema Rajabu.

Kuhusu ushindi alisema haubagui kwani ingekuwa hivyo huenda hata yeye asingekuwa miongoni mwa washindi kwa kuwa hana uhusiano na mahusiano na wahusika zaidi ya akaunti yake ya benki anayoitegemea.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Vijana UVCCM Kagera wataka mwenyekiti wao ajiuzulu

Spread the loveVIJANA wa Chama cha Mapinduzi Mkoa wa Kagera wamemtaka Mwenyekiti...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

THRDC, Wizara ya Katiba wajadili uanzishaji haki binadamu katika biashara

Spread the loveMTANDAO wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania (THRDC), umefanya...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Sitta ang’ang’ana wanafunzi watibiwe bure, Serikali yagoma

Spread the loveMBUNGE wa Urambo, Margaret Sitta, ameishauri Serikali iweke utaratibu wanafunzi...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Waitara ahoji bungeni mwarobaini mauaji katika mgodi Barick North Mara

Spread the loveMBUNGE wa Tarime Vijijini (CCM), Mwita Waitara, ameitaka Serikali kutafuta...

error: Content is protected !!