Rais wa Marekani, Joe Biden ameahidi kufanya ziara barani Afrika, kusini mwa jangwa la Sahara ambayo itakuwa ya kwanza tangu aliposhika wadhifa wake wa urais. Inaripoti Mitandao ya Kimataifa…(endelea).
Rais Biden atafanya ziara hiyo wakati ambapo China na Urusi zinaimarisha uhusiano wa kiuchumi na kijeshi na nchi za Afrika.
Kwenye mkutano na viongozi wa nchi kadhaa za Afrika mjini Washington mapema wiki hii Biden aliahidi vitega uchumi vyenye thamani ya dola bilioni 55 kwa nchi za Afrika katika sekta za biashara na kwa ajili ya misaada ya maendeleo.
Kiongozi huyo wa Marekani pia amependekeza ushiriki wa kudumu wa Umoja wa Afrika kwenye vikao vya kundi la nchi 20 zinazoongoza kiuchumi duniani. Amesema Afrika inastahili kuwa na kiti kwenye kila sehemu.
Leave a comment