Wednesday , 8 May 2024
Home Habari Mchanganyiko 11 waliomuua Wayne Lotter wahukumumiwa kunyongwa
Habari Mchanganyiko

11 waliomuua Wayne Lotter wahukumumiwa kunyongwa

Kitanzi
Spread the love

 

MAHAKAMA Kuu kanda ya Dar es Salaam leo tarehe 2 Disemba, 2022 imewahukumu adhabu ya kunyongwa hadi kufa watu 11 waliokutwa na hatia ya kumuua mwanaharakati wa ujangili, raia wa Afrika Kusini, Wayne Lotter. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Jaji wa Mahakama Kuu Laila Mgonya ametoa hukumu hiyo baada ya kuridhika na ushahidi wa mashtaka uliothibitishwa pasina shaka na mashahidi 32.

Waliohukumiwa ni raia wawili wa Burundi Nduimana Ogiste na Habonimanda Nyandwi pamoja na Watanzania Godfrey Salamba, Rahma Almas,  Chambie Juma Ally, Allan Mafue, Ismail Mohammed, Leonard Makoi, Ayoub Kiholi, Abuu Mkingie, Muchael Kwavava.

Wayne Lotter

Lotter alikuwa Mkurugenzi na Mwanzilishi-mwenza wa Shirika lisilo la kiserikali la PALMS Foundation lilokuwa likijihusisha na mapambano ya ujangili.

Aliuawa tarehe 16 Agosti, 2017 kwa kupigwa risasi na watu waliomvamia akiwa kwenye gari ndogo ya abiria ‘texi’ katika makutano ya barabara za Chole na Haile Selaissie, Masaki wilayani Kinondoni mkoani Dar es Salaam.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

BiasharaHabari Mchanganyiko

NBC, SILABU waungana kufikisha elimu ya fedha majumbani

Spread the loveBenki ya Taifa ya Biashara (NBC) imeingia makubaliano ya ushirikiano...

AfyaHabari MchanganyikoMakala & Uchambuzi

Kisukari cha mimba ni nini?

Spread the loveKisukari cha mimba ni aina ya kisukari kinachotokea kwa baadhi...

Habari Mchanganyiko

Mafunzo kwa bodaboda 395 yamkuna Meya Dodoma

Spread the loveNAIBU Meya wa Jiji la Dodoma, Asma Karama amepongeza mafunzo...

Habari Mchanganyiko

Samia aagiza huduma za dharura maeneo yaliyoathiriwa na kimbunga Hidaya

Spread the love   RAIS wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania, Samia...

error: Content is protected !!