Wednesday , 8 February 2023
Home Kitengo Maisha Elimu Happines Sanga awa mwanafunzi bora ARU
Elimu

Happines Sanga awa mwanafunzi bora ARU

Spread the love
WANAFUNZI 96 wa Chuo Kikuu Ardhi (ARU),   wametunukiwa tuzo mbalimbali kutokana na kufanya vizuri kitaaluma kwa mwaka wa masomo 2021/22. Anaripoti Mwandishi Wetu…(endelea)

Wanafunzi hao walikabidhiwa tuzo hizo leo chuoni hapo na Makamu Mkuu wa chuo hicho, Profesa Evaristo Liwa, kwenye hafla fupi ya kuwapongeza wanafunzi hao.

Mwanafunzi wa kike alibuka mshindi wa jumla ni Happiness Sanga.

Akizungumza kwenye hafla hayo, Naibu Makamu Mkuu wa Chuo, Taaluma, Utafiti na Ushauri, Profesa John Lupala alisema sherehe za kuwazawadia wanafunzi hao kila mwaka zimekuwa zikiwezeshwa na wadau mbalimbali.

Aliwapongeza wadau hao na kuwaomba waendelee kuunga mkono jitihada za wanafunzi hao kwani zawadi mbalimbali zinazotolewa na wadau hao zimekuwa zikisaidia kuongeza ari ya utendaji kazi kwa wanafunzi.

Profesa Lupala alisema tuzo hizo zimekuwa zikisaidia sana kuongeza tija kwenye maisha ya wanafunzi ya kielimu na kiuchumi huko wanakokwenda kufanyakazi.

Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Ardhi (ARU), Profesa Evaristo Liwa akimpa cheti mwanafunzi bora wa mwaka huu wa masomo Happiness Sanga

“Kwenye sherehe za mwaka huu tuna wanafunzi 96, kati yao wasichana ni 50 na wavulana ni 46 ambao wamefuzu kupata tuzo na zawadi mbalimbali kwa vipengele mbalimbali vya kitaaluma,” alisema Profesa Lupala.

Aliwapongeza wanafunzi wote waliopokea tuzo hizo na kuwataka waendelee kuweka jitihada kwenye masomo yao ili waje kuwa mfano wa kuigwa kwa wanafunzi wenzao na jamii kwa ujumla.

Kwa upande wake Makamu Mkuu wa Chuo, Profesa Liwa alisema sherehe za utoaji tuzo Chuoni hapo zitafuatiwa na shughuli ya Mahafali siku ya Jumanne tarehe 6 Desemba ambapo wahitimu 930 wa ARU wa Shahada mbalimbali watatunukiwa Stashahada zao na aliwapongeza kwa kufikia hatua hiyo muhimu kwenye maisha yao.

“Nawapongeza sana wahitimu na baadhi yao wamekuwa wakipokea tuzo mbalimbali kwa miaka kadhaa mfululizo hii inamaanisha kwamba kwenye juhudi ya kweli mafanikio hupatiana ni matumaini ya chuo kuwa juhudi hizo mtaziendeleza kwenye shughuli za ujenzi wa taifa,” alisema

Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Ardhi (ARU), Profesa Evaristo Liwa akimpa cheti mmoja wa wanafunzi wanaohitimu Jumanne

Aliwataja baadhi ya wadau waliotoa tuzo hizo kuwa ni Shirika la Nyumba la Taifa (NHC), Bodi ya Wathamini Tanzania (VRB), Bodi ya Usajili wa Wabunifu na Ukadiriaji Ujenzi (AQRB), African Property Limited, Taasisi ya Wabunifu na Wakadiriaji Ujenzi (TIQS), Mekon na Webb Uronu and Partners.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

ElimuHabari Mchanganyiko

Waliopata Division one St Anne Marie Academy waula, Waahidiwa kupelekwa Ngorongoro, Mikumi

Spread the love WANAFUNZI wa shule ya St Anne Marie Academy waliofanya...

ElimuMakala & Uchambuzi

Waraka maalumu kwa NECTA, “hawapaswi kuungwa mkono”

Spread the loveHATUA iliyotangazwa na Baraza la Taifa la Mitihani (NECTA), ya...

Elimu

NACTVET yafungua dirisha la udahili

Spread the love  BARAZA la Taifa la Elimu ya Ufundi na Mafunzo...

Elimu

Prof. Mwakalila awafunda wanafunzi Chuo Mwalimu Nyerere, “ulipaji ada ni muhimu”

Spread the love  MKUU wa Chuo cha Kumbukumbu cha Mwalimu Nyerere (MNMA),...

error: Content is protected !!