Thursday , 2 February 2023
Home Gazeti Habari CRB yawataka makandarasi kufanya kazi za ubia
Habari

CRB yawataka makandarasi kufanya kazi za ubia

Sehemu ya makandarasi waliohudhuria mafunzo hayo ya siku tatu
Spread the love

BODI ya Usajili wa Makandarasi (CRB), imesema inafurahishwa na kasi ya wanawake wanaojitokeza katika kazi za ukandarasi huku ikiwataka makandarasi wa ndani kuwa makini kwenye usimamizi wa fedha.

Hayo yalisemwa mwishoni mwa wiki na Mwenyekiti wa Bodi hiyo, Mhandisi Consolata Ngimbwa, wakati wa kufunga mafunzo ya siku tatu kuhusu usimamizi wa fedha kwa makandarasi wa ndani, yaliyoandaliwa na Bodi hiyo jijini Dar es Salaam.

Alisema hata mafunzo hayo yaliyohudhuriwa na washiriki 163 idadi kubwa ni wanawake hali ambayo inatia matumaini kwamba wanawake wameanza kuona fursa kwenye kazi hizo.

Alisema mafunzo hayo ni muhimu kwani bila usimamizi mzuri wa fedha uwezekano wa kutekeleza miradi kikamilifu unakuwa mdogo na hata ukikamilika unakosa unafisi.

“Nimeambiwa kwamba katika mafunzo ya usimamizi wa fedha mlijikita katika uelewa wa taarifa za fedha namna ya kufanya maamuzi ya fedha kwa kuzingatia hali halisi ya taarifa za fedha na usimamizi wa mitaji haya ni mambo muhimu sana kwa mkandarasi yoyote,” alisema

“Mmejifunza pia masuala ya kodi hasa namna nzuri ya kutunza kumbukumbu ili kuepuka kodi zisizostahili au faini kama adhabu kwa kukiuka misingi muhimu ya  uandaaji wa mahesabu ya fedha za kampuni,” alisema

Mwenyekiti wa Bodi ya Usajili wa Makandarasi (CRB), Consolata Ngimbwa akizungumza wakati wa kufunga mafunzo ya siku tatu kwa makandarasi wa ndani kuhusu usimamizi wa fedha, mafunzo yaliyofanyika jijini Dar es Salaam.

Aidha, alisema ujuzi wa kutumia mifumo ya kielektroniki kama mfumo wa manunuzi wa TANePS ni muhimu na mkandarasi ambaye atashindwa kujifunza mfumo huo hawezi kufika mbali kwani mwajiri mkubwa ni serikali ambaye huytoa zabuni zote kwa njia ya kielektroniki.

Mhandisi Ngimbwa aliwasisitiza pia makandarasi kuacha ubinafsi na kuchangamkia miradi mikubwa ya ubia hali ambayo itawapa fursa ya kukua kitaalamu na kiuchumi.

“Kutimiza masharti ya zabuni kubwa ni vigumu kwa wengi wetu tunaposhiriki tukiwa mmoja mmoja lakini kwa mfumo wa ubia tunaweza kuyatimiza masharti hayo na kushindana vizuri,” alisema

Aliwataka pia makandarasi kushikamana na kuunganisha nguvu ili kuwa na sauti moja ambayo itakuwa na uwezo wa kukabiliana na changamoto mbalimbali zinazowakabili.

Aidha, aliwakumbusha makandarasi kujiepusha na vitendo vya kutoa na kupokea rushwa na kuwataka watoe taarifa kwenye vyombo vya usalama pale wanapoombwa rushwa na watoa zabuni.

“Tukifanyakazi kwa kuzingatia weledi na maadili suala la rushwa halitakuwa na nafasi miongoni mwetu tukikubali kubadilika sote tutaibadilisha sekta yetu ya ukandarasi,” alisema

Naibu Msajili wa bodi ya Usajili wa Makandarasi CRB, Mhandisi David Jere akizungumza kwenye hafla ya kufunga mafunzo ya siu tatu kwa makandarasi wa ndani yaliyofanyika jijini Dar es Salaam.

Naye Naibu Msajili, Utafiti na Maendeleo, Mhandisi David Jere alisema makandarasi waliopata mafunzo wametoka mikoa ya Dar es Salaam, Morogoro, Mtwara, Arusha, Pwani, Lindi, Dodoma, Mwanza, Rukwa, Ruvuma, Songwe, Iringa, Kagera, Katavi, Kigoma, Manyara, Mara, Mbeya, Tanga na Zanzibar.

Alisema lengo la mafunzo hayo ni kuwajengea misingi itakayowasaidia kusimamia rasilimali fedha vizuri na kutunza kumbukumbu vizuri ili kuepuka kodi zisizostahili au faini kwa kushindwa kuandaa vyema hesabu za kampuni.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

HabariHabari Mchanganyiko

CRB yashtukia makandarasi wanaofanya ubia wa ujanja ujanja, yasema watakaobainika kuchukuliwa hatua kali

Spread the love  BODI ya Usajili wa Makandarasi (CRB), imeonya makandarasi wanaofanya...

HabariKimataifa

Aliyesomeshwa na mchumba aamuriwa kurudisha Sh 9.4 Mil. baada ya kukataa kuolewa

Spread the love  MWANAMKE mmoja nchini Uganda ambaye aliuumiza moyo wa mchumba...

Habari

Mnyika aacha ujumbe msibani kwa kada wa Chadema aliyefia vitani Ukraine

Spread the loveKATIBU Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo-Chadema Taifa, John...

HabariHabari Mchanganyiko

Mwili wa kada wa Chadema aliyefia vitani Ukraine wawasili, kuzikwa Mbeya

Spread the loveMWILI wa Kada wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo-Chadema, aliyefia...

error: Content is protected !!