Friday , 3 May 2024
Home Habari Mchanganyiko 19 wafariki dunia ajali ya ndege Bukoba
Habari MchanganyikoTangulizi

19 wafariki dunia ajali ya ndege Bukoba

Spread the love

WATU 19 wakiwemo abiria na wahudumu wamefariki dunia katika ajali ya ndege ya shirika la Ndege la Precision Air iliyotokea asubuhi ya leo Jumapili tarehe 6 Novemba, 2022 katika Ziwa Victoria Mkoani Kagera. Anaripoti Mwandishi Wetu …(endelea).

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ametangaza vifo vya watu 19 wakiwemo abiria na wahudumu katika ajali ya ndege ya shirika la Ndege la Precision Air iliyotokea asubuhi ya leo Jumapili tarehe 6 Novemba , 2022 katika Ziwa Victoria Mkoani Kagera.

Majaliwa ametangaza vifo hivyo leo jioni ikiwa ni saa chache baada ya kuwasili kwenye eneo ilipotokea ajali hiyo.

Kwa mujibu wa Mkuu wa mkoa huo, Albert Chalamila, ndege hiyo Precision Air ATR 42 SH PWF ilikuwa na watu 43, kati yao 39 wakiwa abiria, marubani wawili na wahudumu wawili ambapo tayari 28 wameokolewa.

Taarifa hiyo ya Waziri Mkuu imekuja ikiwa ni saa chache baada ya Mganga Mkuu wa Mkoa wa Kagera, Issessanda Kaniki kuthibitisha kutokea kwa vifo vya watu watatu.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Chadema waendelea kulilia katiba mpya

Spread the loveCHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimeendelea kudai upatikanaji wa...

Habari za SiasaTangulizi

Chadema kumshtaki Rais Samia

Spread the loveCHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimetishia kumfungulia kesi ya...

BiasharaHabari Mchanganyiko

NMB yang’ara maonesho OSHA

Spread the loveBenki ya NMB imebeba tuzo ya kampuni bora kwenye sekta...

Habari MchanganyikoKimataifa

Ruto amteua Kahariri kuwa mkuu wa majeshi

Spread the loveRAIS wa Kenya, William Ruto, amemteua Jenerali Charles Muriu Kahariri,...

error: Content is protected !!