Saturday , 27 April 2024
Home Habari Mchanganyiko Majaliwa awajulia hali manusura ajali ta ndege Bukoba
Habari Mchanganyiko

Majaliwa awajulia hali manusura ajali ta ndege Bukoba

Spread the love

 

WAZIRI Mkuu Kassim Majaliwa amewasili mkoani Kagera kushuhudia zoezi la uokoaji wa Ndege ya Shirika la Precision Air iliyopata ajali katika Ziwa Victoria, Bukoba mkoani Kagera iliyopata ajali leo Jumapili mkoani Kagera. Anaripoti Mwandishi Wetu, Bukoba …(endelea).

Majaliwa amewajulia hali wahanga wa ajali wanaopata matibabu katika hospitali ya Mkoa wa Kagera.

Akizungumza katika eneo hilo amesema kuwa Rais Samia Suluhu Hassan ametoa pole kwa watu wote walioguswa na ajali hiyo na kwamba Serikali itaendelea kutoa huduma stahiki kwa majeruhi wote.

Pia amewataka wananchi kuwa na subira katika kipindi hiki ambacho Serikali itafanya uchunguzi kupitia vyombo vyake ili kubaini chanzo cha ajali hiyo.

Mganga Mkuu wa Mkoa wa Kagera, Issessanda Kaniki amethibitisha kutokea kwa vifo vya watu 19. Ndege hiyo ilikuwa ikitoka Dar es Salaam kwenda Bukoba.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Wakili: Ukimpa zawadi mwenza marufuku kumpora hata mkiachana

Spread the love  WANANDOA na watu waliko kwenye mahusiano ya kimapenzi, wamekumbushwa...

Habari Mchanganyiko

Majaliwa: Mvua zimesababisha vifo vya watu 155, kuendelea hadi Mei

Spread the love  WAZIRI Mkuu, Kassim Majaliwa amesema mvua kubwa za El-Nino...

Habari Mchanganyiko

Exim Bank yatoa  vitanda kwa shule ya Jeshi la Polisi Moshi

Spread the love  BENKI ya Exim imekabidhii  seti ya vitanda kwa Shule...

Habari Mchanganyiko

NBC yakabidhi vitanda Shule ya Polisi Moshi

Spread the loveBenki ya NBC imekabidhi msaada wa vitanda 28 kwa Shule...

error: Content is protected !!