December 2, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Majina 19 waliofariki ajali ya ndege Bukoba yatajwa, wamo Rubani na msaidizi wake

Ndege ya Precision ikiwa imezama katika ziwa Victoria baada ya kushindwa kutua uwanja wa Ndege wa Bukoba, Kagera

Spread the love

 

MAJINA ya watu 18 kati ya 19 waliofariki katika ajali ya ndege ya Precision Air iliyotokea leo Jumapili asubuhi katika Ziwa Victoria wilayani Bukoba mkoani Kagera, yametajwa. Anaripoti Mwandishi Wetu, Bukoba  … (endelea).

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa jioni ya leo tarehe 6 Novemba, 2022 na Mkuu wa mkoa wa Kagera, Albert Chalamila kati ya waliofariki wamo pia rubani wa ndege hiyo, Buruani Lubaga na msaidizi wake, Peter Odhiambo ‘First officer’

Ndege hiyo yenye usajili 5H -PWF ilikuwa imebeba jumla ya watu 43 ambao 39 ni abiria, marubani wawili na wahudumu wawili, ilikuwa ikitokea Dar es Salaam kuelekea Bokoba.

Aidha, kwa mujibu wa taarifa hiyo majina ya wengine 16 waliofariki ni Atulinde Biteya, Aneth Biteya, Neema Faraja, Hanifa Hamza, Aneth Kaaya, Victor Lauren, Said Malat Lyangana na
Iman Paul.

Wengine ni Faraji Yusuph, Lin Zhang, Sauli Epimark, Zacharia Mlacha, Eunice Ndirangu, Mtani Njegere, Zaitun Shillah na Dk. Alice Simwinga.

Aidha, Chalamila amesema athari nyingine zilizotokana na ajali hiyo ni baadhi ya safari kuahirishwa.

Amesema ndege ya ATCL iliyopaswa kwenda Bukoba leo iliahirishwa kutokana na kiwanja cha kufungwa hivyo abiria kupelekwa hotelinu hadi kesho.

Aidha, abiria waliopaswa kusafiri kwa ndege ya Precision Air kuelekea Dar es Salaam wamesafirishwa kwa ndege ya ATCL na wengine kwa ndege ya ya Precision Air kuelekea Dar es Salaam kipitia Kilimanjaro.

Ameongeza kuwa timu ya uchunguzi wa ajali za ndege kutoka TCAA imeshafika Bukoba tayari kwa uchunguzi.

error: Content is protected !!