Thursday , 2 May 2024
Home Habari Mchanganyiko Mtoto mchanga ni miongoni mwa abiria waliopata ajali-Precision
Habari Mchanganyiko

Mtoto mchanga ni miongoni mwa abiria waliopata ajali-Precision

Ndege ya Precision ikiwa imezama katika ziwa Victoria baada ya kushindwa kutua uwanja wa Ndege wa Bukoba, Kagera
Spread the love

KAMPUNI ya ndege ya Precision imetoa taarifa ya uwepo wa mtoto mchanga mmoja miongoni mwa abiria 39 waliokuwa kwenye ndege iliyopata ajali Bukoba mkoani Kagera na kutumbukia Ziwa Victoria leo Jumapili tarehe 6 Novemba, 2022. Anaripoti Jonas Mushi, Dar es Salaam…(endelea)

Taarifa hiyo ambayo ni ya pili kwa umma iliyotolewa na kampuni hiyo imesema abiria wengine 38 ni watu wazima. Kampuni hiyo imesema watu 26 wameokolewa hadi sasa katika ajali hiyo lakini haijaweka wazi kama kichanga hicho ni miongoni mwao.

Taarifa hiyo ya Precision iliyowekwa kwenye mitandao wake ya kijamii, imesema hakuna vifo vilivyodhibitishwa hadi sasa na imetuma timu ya uchunguzi inayoundwa na maofisa wake na wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA) kuungana na timu ya uokozi. Kampuni hiyo itazungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam saa 9 kamili alasiri kuhusu ajali hiyo.

Ndege hiyo mruko namba PW 494 ilikuwa ikitokea jijini Dar es Salaam kuelekea Bukoba, imepata ajali na kutumbukia Ziwa Victoria asubuhi ya leo ikiwa na watu 43 miongonimwao abiria 39, wahudumu wawili na marubani wawili.

Taarifa ya awali iliyotolewa na Mkuu wa Mkoa wa Kagera imeeleza zoezi la ukoaji linaendelea na kuna mawasiliano na marubani waliopo ndani ya ndege hiyo namba ATR-48 yenye usajili namba 5H-PWF.

 

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Chadema waendelea kulilia katiba mpya

Spread the loveCHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimeendelea kudai upatikanaji wa...

BiasharaHabari Mchanganyiko

NMB yang’ara maonesho OSHA

Spread the loveBenki ya NMB imebeba tuzo ya kampuni bora kwenye sekta...

Habari MchanganyikoKimataifa

Ruto amteua Kahariri kuwa mkuu wa majeshi

Spread the loveRAIS wa Kenya, William Ruto, amemteua Jenerali Charles Muriu Kahariri,...

Habari Mchanganyiko

Chongolo aonya viongozi vijiji kutouza NIDA kwa wageni

Spread the loveMKUU wa Mkoa wa Songwe, Daniel Chongolo amewaonya viongozi wa...

error: Content is protected !!