Tuesday , 30 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Matokeo ya Sensa 2022: Idadi ya watu Tanzania yafikia Mil. 61.7
Habari za SiasaTangulizi

Matokeo ya Sensa 2022: Idadi ya watu Tanzania yafikia Mil. 61.7

Rais Samia Suluhu Hassan
Spread the love

 

RAIS wa Tanzania Samia Suluhu Hassan ametangaza kuwa idadi ya Watanzania imefikia milioni 61.7 kufikia tarehe 31 Oktoba 2022. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dodoma … (endelea).

Mkuu huyo wa nchi ametangaza idadi hiyo leo Jumatatu tarehe 31 Oktoba, 2022 , katika uzinduzi rasmi wa matokeo ya sensa ya watu na makazi ya mwaka 2022 uliofanyika jijini Dodoma.

“Ninawatangazia rasmi kuwa Tanzania ina idadi ya watu wapatao 61,741,120,” amesema Rais Samia.

Kati ya idadi hiyo 59,851,357 wapo Tanzania bara na watu 1,889,773 ni kutoka Zanzibar. Ripoti hiyo imeonesha kuwa idadi ya wanawake ni 31,687,990 sawa na asilimia 51, huku wanaume wakiwa 30,053,130 sawa na asilimia 49 ya watu wote.

Kwa kipindi cha miaka 10 iliyopita Tanzania ilikuwa na idadi ya watu 44,928,923 hii inaonesha kumekuwepo na ongezeko la watu 16,812,197 sawa na ongezeko la 3.2% kati ya ongezeko la mwaka 2012 na mwaka 2022.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo mwaka 2022 bara la Afrika hususani katika nchi zilizo kusini mwa jangwa la Sahara lina jumla ya watu bilioni 1.2 idadi inayokadiriwa kuongezeka hadi kufikia watu bilioni 2.1 ifikapo mwaka 2050.

12 Comments

  • Naona watanzania tuongeze bidii ya kuzaliana ili kutengeneza soko letu la ndani kwa bidhaa zinazozalishwa na wazawa!

  • Hongera watanzania wore waliojali na kujitoa ili kuhesabiwa👏👏
    Hii inatuonesha nini kifanyike kulinda na kuongeza maendeleo tuliyo nayo kila nyanja.

  • Naomba Idadi ya wazee kuanzia 50 hadi 60 61 hadi 70 71 hadi 80 81 hadi 90, na 91 ha 100 wanawake wangapi nawanaume wangapi

  • Shime sasa kwa waTanzania wote. Ongezeko hili la watu liende sambamba na uboreshaji wa secta za Elimu, Afya, Miundombinu na Makazi kwakuziendeleza secta hizo ktk nyanja zake husika

  • Inapendeza sana , Tubadilishe sasa miundo mbinu na sekta zote watu wapate nafas za ajira na namna ya kujiajiri. Najua vijana ni weng zaidi katika umati huo lakn Serikali ianze sasa kuwajali vjana

  • Hongera mama kwa Jambo kwa kwakuwatambua wananchi wako idadi bila shaka ni njambo la Kujivunia sana
    Naipenda tanzania 🇹🇿🇹🇿🇹🇿🇹🇿🇹🇿🇹🇿

  • Hongera the Rais wetu mama Samia suluhu Hassan Kwa kuhakikisha sensa inafanyika na wa Tanzania na dunia Kwa jumla tunapata matokeo ya idadi yetu sote Kwa wakati,

  • Hongera mh. Samia s hasan kwa kumaliza salama jukum hilo zito hivyo tunaomba simamia barabara wizara zote zitekeleze bajet zake vilivyo kwa watanzania ili kupunguza ugumu wa watanzania tajili wa nchi yao na bunge litambue vilvyo uongezekaj wa idadi hio kubwa ya watu MTNGU AKUPE MAISHA MALEFU NA AKUPE HEKIMA YA UONGOZ AMEN.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaTangulizi

Dk. Slaa: Watanzania iungeni mkono Chadema uchaguzi 2025

Spread the loveMWANASIASA mkongwe nchini Tanzania, Dk. Wilbroad Slaa, amewataka watanzania wakiunge...

Habari za SiasaTangulizi

Samia ataja miradi ambayo Tanzania inashirikiana na IDA

Spread the loveRais wa Tanzania Dk. Samia Suluhu Hassan leo Jumatatu amehutubia...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

7 wafa Ulanga, mbunge alia kutelekezwa na mawaziri, Tanroad

Spread the loveWatoto saba wamepoteza maisha na zaidi ya kaya 70 kukosa...

Habari za SiasaTangulizi

Wizara Katiba na Sheria yaliomba Bunge Sh. 441.2 bilioni

Spread the love  WIZARA ya Katiba na Sheria imeliomba Bunge liidhinishe bajeti...

error: Content is protected !!