Tuesday , 30 April 2024
Home Habari Mchanganyiko RC Makala: Lita milioni 70 zinaingizwa mjini kupunguza mgawo wa maji
Habari Mchanganyiko

RC Makala: Lita milioni 70 zinaingizwa mjini kupunguza mgawo wa maji

Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Amos Makalla
Spread the love

 

MKUU wa mkoa wa Dar es Salaam, Amos Makalla leo Jumanne ametangaza kwamba leo usiku lita milioni 70 za maji zitaingizwa katika visima 12 vilivyojengwa eneo la Kigamboni ili kupunguza makali ya mgawo wa maji katika mkoa huo. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Makala ametoa kauli hiyo leo tarehe 1 Novemba, 2022 jijini Dar es Salaam wakati akitoa taarifa kwa Rais Samia Suluhu Hassan kuhusu maagizo aliyompatia kuhakikisha ndani ya wiki mbili mradi wa maji Kigamboni unakamilika.

Akitoa salamu za mkoa huo mbele ya Rais Samia ambaye ni amefungua kongamano la nishati safi ya kupikia, Makala amesema kukamilika kwa mradi huo kumetokana na fedha Sh bilioni 23 zilizotolewa na serikali kuharakisha utekekezaji wake.

“Nina furaha kuripoti kwako (Rais Samia) kwamba usiku wa leo tunaingiza maji kutoka Kigamboni katika visima 12 ambavyo vimetokana na Sh bilioni 23 ulizotoa na sasa lita milioni 70 zitaingia mjini ili kupunguza ukali wa mgawo wa maji,” amesema.

Amesema tatizo la mgawo wa maji ni ukame ambao umetokana na uhaba wa mvua za vuli ambao pia Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) ilitangaza ukame.

“Kwa hiyo chanzo cha ukame ni kudra za Mwenyezi Mungu na wala sio ilani ya CCM.

“Ili kuondokana na tatizo la muda mrefu la maji… uliagiza na ninaripoti kwako kwamba ule mradi tuliosubiri miaka mingi la bwawa la Kidunda, mkataba wake umesainiwa jana. Kwa hiyo ndio itakuwa suluhu ya kuhifadhi maji ambapo mvua zikipungua maji hayo yatafunguliwa,” amesema.

Aidha, akizungumzia kuhusu kongamano hilo la nishati, Makala amesema mkoa wa Dar es salaam ambao kwa mujibu wa matokeo ya sensa ya mwaka 2022 ndio wenye idadi kubwa ya watu sawa na asilimia nane ya Watanzania wote, utakuwa kinara Kusimamia na kutumia nishati safi.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

TMA yapongezwa kuimarisha ubora na usahihi wa taarifa za Hali ya Hewa

Spread the love  WAFANYAKAZI wa Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA),...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

7 wafa Ulanga, mbunge alia kutelekezwa na mawaziri, Tanroad

Spread the loveWatoto saba wamepoteza maisha na zaidi ya kaya 70 kukosa...

Habari Mchanganyiko

Bil 12.4 zimetumika ujenzi wa miradi wilaya ya Momba

Spread the love MKUU wa wilaya ya Momba mkoani Songwe Kennan Kihongosi...

AfyaHabari Mchanganyiko

Songwe katika mikakati ya elimu ya lishe kudhibiti udumavu

Spread the love  SERIKALI mkoani Songwe imejipanga kuendelea kutoa elimu ya lishe...

error: Content is protected !!