December 5, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Matokeo ya Sensa 2022: Idadi ya watu Tanzania yafikia Mil. 61.7

Rais Samia Suluhu Hassan

Spread the love

 

RAIS wa Tanzania Samia Suluhu Hassan ametangaza kuwa idadi ya Watanzania imefikia milioni 61.7 kufikia tarehe 31 Oktoba 2022. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dodoma … (endelea).

Mkuu huyo wa nchi ametangaza idadi hiyo leo Jumatatu tarehe 31 Oktoba, 2022 , katika uzinduzi rasmi wa matokeo ya sensa ya watu na makazi ya mwaka 2022 uliofanyika jijini Dodoma.

“Ninawatangazia rasmi kuwa Tanzania ina idadi ya watu wapatao 61,741,120,” amesema Rais Samia.

Kati ya idadi hiyo 59,851,357 wapo Tanzania bara na watu 1,889,773 ni kutoka Zanzibar. Ripoti hiyo imeonesha kuwa idadi ya wanawake ni 31,687,990 sawa na asilimia 51, huku wanaume wakiwa 30,053,130 sawa na asilimia 49 ya watu wote.

Kwa kipindi cha miaka 10 iliyopita Tanzania ilikuwa na idadi ya watu 44,928,923 hii inaonesha kumekuwepo na ongezeko la watu 16,812,197 sawa na ongezeko la 3.2% kati ya ongezeko la mwaka 2012 na mwaka 2022.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo mwaka 2022 bara la Afrika hususani katika nchi zilizo kusini mwa jangwa la Sahara lina jumla ya watu bilioni 1.2 idadi inayokadiriwa kuongezeka hadi kufikia watu bilioni 2.1 ifikapo mwaka 2050.

error: Content is protected !!