Friday , 26 April 2024
Home Kitengo Maisha Elimu Dk. Mwinyi mgeni rasmi kongamano la uchumi na biashara la CBE
ElimuHabari

Dk. Mwinyi mgeni rasmi kongamano la uchumi na biashara la CBE

Mkuu wa Chuo cha Elimu ya Biashara, (CBE), Profesa Emmanuel Mjema akizungumza na waandishi wa habari kuhusu kongamano la kitaaluma litakalofanyika Dodoma hivi karibuni. Kushoto ni Naibu Mkuu wa chuo Taaluma, Profesa Tandi Lwoga na kulia ni Naibu Mkuu wa chuo, anayeshughulikia Mipango na Fedha Dk. Emmanuel Munishi.
Spread the love

CHUO cha Elimu ya Biashara (CBE), kimeandaa kongamano la maendeleo ya biashara na uchumi ambalo linatarajaiwa kufunguliwa na Rais wa Zanzibar Dk. Hussein Ali Mwinyi mkoani Dodoma. Mwandishi Wetu

Hayo yalisemwa jana chuoni hapo na Mkuu wa chuo hicho, Profesa Emmanuel Mjema, wakati akizungumzia kongamano hilo litakalofanyika tarehe 15 na 16 mwezi huu kwenye ukumbi wa mikutano wa Jakaya Kikwete mkoani humo.

Alisema kongamano hilo linakauli mbiu ya ‘Biashara Uwekezaji na Ubunifu kwa Mabadiliko ya Kiuchumi na kwamba kutokana na umuhimu wake viongozi mbalimbali wa Tanzania bara na visiwani watashiriki kongamano hilo.

Profesa Mjema alitaja mada zitakazojadiliwa kwenye kongamano hilo kuwa ni pamoja na  Biashara ya ndani na kimataifa, Uwekezaji wa moja kwa moja wa kigeni, Ubunifu na Ujasiriamali, Uwezeshaji wa Biashara na Ushirikiano wa Kiuchumi, uwekezaji na Teknolojia, Uchumi wa Buluu, Zuia mnyororo na Fedha za kidijitali

Profesa Mjema alisema lengo la mdahalo huo wa Kitaaluma ni kujenga uwezo na mitandao miongoni mwa watafiti na wadau wengine barani Afrika na kutoa fursa ya kuleta maendeleo ya kiuchumi kupitia biashara na kwamba kongamano hilo litasaidia kuleta ufahamu mpya katika tasnia mbalimbali.

Pia Profesa Mjema alisema kutakuwa na mahafali ya 57 ya CBE ambapo mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Waziri Mkuu Kassim Majaliwa Novemba 12 mwaka huu katika kampasi ya Dar es Salam ambapo kutakuwa na wahitimu wa Shahada ya Uzamili, Stashahada ya Uzamili, Shahada ya Kwanza, Stashahada na Cheti cha Ufundi.

NAIBU Mkuu wa Chuo cha Elimu ya Biashara Taaluma, Profesa Tandi Lwoga akizungumza kuhusu mahafali ya chuo hicho yanayotarajiwa kufanyika mwezi huu na kongamano la biashara litakalofanyika mkoani Dodoma. Katikati ni Mkuu wa chuo hicho, Profesa Emmanuel Mjema na Kulia ni Naibu Mkuu wa chuo Mipango na Fedha Dk Emmanuel Munishi.

Alisema wiki ya Makongamano kwa Kampasi zote shughuli zitaanza Jumatatu hadi Alhamis ambayo itakuwa ni siku ya kilele na kwamba katika wiki hiyo shughuli mbalimbali kama vile mawasilisho ya machapisho, maonesho ya Idara za Kitaaluma ambayo yawahusisha wahitimu wa zamani yaani CBE Alumni ambao wanakaribishwa kuonesha bidhaa na huduma wanazozifanya.

“Pia semina na warsha kuhusu mambo mbalimbali ya biashara zitawezeshwa bila gharama yoyote na katika mahafali hayo ya 57 katika Kampasi zetu zote takribani Wahitimu 2,000 watatunukiwa stahiki zao katika ngazi tofauti tofauti,” alisema Profesa Mjema

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

ElimuHabari za Siasa

MbungeCCM ataka kasi uzalishaji walimu ipunguzwe akidai hakuna ajira

Spread the love  MBUNGE wa Mlalo (CCM), Rashid Shangazi, ameishauri Serikali ipunguze...

ElimuHabari za Siasa

Walimu 52,551 kupandishwa madaraja mwaka huu

Spread the loveNaibu Waziri wa nchi, Ofisi ya Rais (Utumishi na Utawala...

BiasharaElimu

NMB yatoa vifaa vya ujenzi kwa shule sita Nyasa  

Spread the loveBENKI ya NMB imetoa msaada wa vifaa mbalimbali vya ujenzi...

ElimuHabari Mchanganyiko

GGML yawapa mbinu wanafunzi Geita Boys kufikia malengo ya kitaaluma

Spread the loveKampuni ya Geita Gold Mining Limited (GGML) imetoa mafunzo maalumu...

error: Content is protected !!