December 5, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Shaka: Rais Samia aungwe mkono bila kujali itikadi za kisiasa

Katibu wa Itikadi na uenezi CCM, Shaka Hamidu Shaka

Spread the love

 

KATIBU wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya CCM Itikadi na Uenezi, Shaka Hamdu Shaka, amesema ni jukumu la Watanzania wote kumuunga mkono Rais Samia Suluhu Hassan kutokana na kazi kubwa anayoifanya kuleta maendeleo nchini. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dodoma … (endelea).

Shaka ameyasema hayo akiwa Msalato mkoani Dodoma alipokuwa akijibu maswali ya waandishi wa habari waliotaka kujua ni kwa kiasi gani CCM inaridhishwa na utekelezaji wa Ilani yake ya Uchaguzi (2020-2025 baada ya Rais Samia kuweka jiwe la msingi la ujenzi wa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Msalato mkoani humo.

“Wote tuna jukumu la kujenga nchi bila ya kuangalia itikadi zetu za kisiasa, haya yanayofanyika ni kwa maslahi mapana ya Watanzania. Ni imani yetu kwamba wenzetu wa vyama vingine wataunga mkono jitihada hizi.

“Ni kweli Ilani inayotekelezwa ni ya Chama Cha Mapinduzi lakini maendeleo yanayoletwa ni ya Watanzania wote kwa ujumla, kwa hiyo nitoe wito tumeanza vizuri, Mheshimiwa Rais Samia tangu ameingia madarakani ametuunganisha pamoja, tunakwenda vizuri kikubwa ni kuendelea kusisitiza kuwa umoja wetu ndio ushindi wetu,” amesema.

Aidha, Shaka amesema kuimarika kwa ujenzi wa miradi ya kimkakati ni kufungua fursa za kiuchumi kwa Watanzania hivyo ni ana imani kwamba wananchi watatumia vyema fursa ambazo zinatolewa na serikali ya Chama Cha Mapinduzi.

error: Content is protected !!