Wednesday , 8 May 2024
Home Habari Mchanganyiko IGP awasimamisha kazi askari waliohusika mauji Kilombero kupisha uchunguzi
Habari Mchanganyiko

IGP awasimamisha kazi askari waliohusika mauji Kilombero kupisha uchunguzi

IGP, Camilius Wambura
Spread the love

MKUU wa Jeshi la Polisi nchini Tanzania, IGP Camillus Wambura, amewasimamisha kazi askari wote waliohusika na tukio la mauji ya raia wawili yaliyotokea tarehe 23 Oktoba, 2022 katika Kijiji cha Ikwambi Kata ya Mofu wilayani Kilombero mkoani Morogoro, ili kupisha uchunguzi. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Mauji hayo yalitokea kufuatia vurugu za wananchi jamii ya wafugaji na wakulima ambao walikuwa wanalalamikia mifugo kuingizwa kwenye mashamba yao na wenzao wawili kushambuliwa.

Kwa mujibu wa taarifa ya IGP Wambura aliyoitoa leo Jumatatu tarehe 24 Oktoba, 2022, amesema ameunda timu ya uchunguzi itakayoongozwa na Mkurugenzi wa Mashitaka  pamoja na taasisi zingine za Serikali ili kufanya uchunguzi huru.

Amesema katika taarifa yake hiyo kuwa lengo la uchunguzi huo ni kupata majibu ya chanzo cha tukio hilo na kubaini uwiano wa matumizi ya nguvu iliyotumiwa na Jeshi la Polisi katika kudhibiti vurugu na endapo zilienda sambamba na vurugu zenyewe.

“Nimeelekeza kuwa askari wote waliohusika kwenye tukio hilo wakae kando kupisha uchunguzi ili timu hii huru iwe na nafasi nzuri ya kuweza kutimiza wajibu wake na kuweza kuja na majibu na matokeo sahihi ya uchunguzi huo kwa jamii ili Watanzania waweze kufahamu ukweli wa tukio hilo.

“Endapo  kutabainika mapungufu, madhaifu au chochote kile amabcho kinaonesha uzembe kwa upande wa yeyote yule, basi hatua stahiki za kisheria zitachukuliwa dhidi yake,” amesema Wambura.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

BiasharaHabari Mchanganyiko

NBC, SILABU waungana kufikisha elimu ya fedha majumbani

Spread the loveBenki ya Taifa ya Biashara (NBC) imeingia makubaliano ya ushirikiano...

AfyaHabari MchanganyikoMakala & Uchambuzi

Kisukari cha mimba ni nini?

Spread the loveKisukari cha mimba ni aina ya kisukari kinachotokea kwa baadhi...

Habari Mchanganyiko

Mafunzo kwa bodaboda 395 yamkuna Meya Dodoma

Spread the loveNAIBU Meya wa Jiji la Dodoma, Asma Karama amepongeza mafunzo...

Habari Mchanganyiko

Samia aagiza huduma za dharura maeneo yaliyoathiriwa na kimbunga Hidaya

Spread the love   RAIS wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania, Samia...

error: Content is protected !!