Wednesday , 8 February 2023
Home Kitengo Michezo Benki ya NBC ilivyoipamba Derby ya Kariakoo
Michezo

Benki ya NBC ilivyoipamba Derby ya Kariakoo

Spread the love

BENKI ya Taifa ya Biashara (NBC) ambae ni mdhamini Mkuu wa Ligi Kuu ya Soka ya Tanzania Bara, NBC Premiere League jana iliipamba mechi ya watani wa jadi katika soka la Tanzania kati ya Yanga na Simba kwa kuandaa matukio kadhaa kwa ajili ya wapenzi wa mchezo huo ikiwemo wateja wake wakubwa na wadogo sambamba na kukabidhi tuzo na zawadi kwa mchezaji bora wa ligi hiyo kwa mwezi Septemba. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Shughuli zote hizo ziliongozwa na maofisa waandamizi wa benki hiyo wakiongozwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki hiyo, Theobald Sabi ambae alipata wasaa wa kukabidhi tuzo na zawadi ya fedha kiasi cha sh mil 1, kwa mchezaji wa klabu ya Yanga, Feisal Salum alietangazwa mchezi bora wa ligi hiyo kwa mwezi Septemba.

Tukio hilo lililoshuhudiwa na maelfu ya mashabiki waliojitokeza kutazama mechi hiyo katika Uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam, lilitanguliwa na matukio mengine ambapo benki hiyo iliandaa mwaliko rasmi kwa ajili ya wateja wake wakubwa zaidi ya 50 waliopata wasaa kupata chakula cha mchana pamoja na viongozi wa benki ya NBC kisha kwa pamoja walielekea Uwanja wa Taifa kushudia mechi hiyo wakiwa katika msafara maalum.

Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Taifa ya Biashara (NBC) ambae ni mdhamini Mkuu wa Ligi Kuu ya Soka ya Tanzania Bara, NBC Premiere League Bw Theobald Sabi (Kulia) akikabidhi tuzo kwa mchezaji wa klabu ya Yanga Feisal Salum alietangazwa mchezaji bora wa ligi hiyo kwa mwezi Septemba

Akizungumzia hatua ya benki hiyo, Kaimu Mkuu wa Idara ya Masoko wa Benki hiyo, David Kigwile alisema mbali na wateja wakubwa, benki hiyo pia ilitoa tiketi 70 kwa ajili ya wateja wake wadogo wa tawi jipya la Kigamboni ili waweze kwenda kutazama mtanange huo ikiwa ni ishara ya kuwakaribisha waweze kufurahia huduma za benki hiyo wilayani humo.

“Tumetumia mechi hii kubwa kuwakaribisha wateja wetu wa tawi letu jipya lililopo wilayani Kigamboni lengo likiwa ni kufurahi nao katika mchezo huu pendwa. Zaidi ya wateja 70 wilayani humo walipata fursa ya kutazama mechi hiyo kwa udhamini wa benki ya NBC ambapo tuliweza kuwakatia tiketi wote pamoja na kuwapatia usafiri wa kwenda uwanjani na kurudi majumbani mwao wakiwa salama kabisa,’’ alisema.

Aidha, benki hiyo iliandaa ‘Screen’ kubwa kwenye baadhi ya maeneo wilayani humo ili kutoa fursa kwa wapenzi wa mchezo huo ambao hawakuweza kufika uwanjani ili waweze kufurahia mechi hiyo.

“Mbali na kutoa fursa kwa wapenzi wa soka kufuatilia mechi hiyo kupitia screen kubwa pia walipata fursa ya kupata huduma mbalimbali za kifedha kutoka benki ya NBC kupitia maofisa wetu waliokuwa wakitoa huduma mbalimbali ikiwemo kufungua akaunti mbalimbali pamoja na kufanya mihamala ya kifedha wakiwa maeneo hayo pamoja na viunga vya vya uwanja wa Benjamin Mkapa,” alisema.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Michezo

GGML: Uwanja mpya wa Geita Gold FC kukamilika Mei, 2023

Spread the loveUWANJA wa Magogo unaojengwa na Halmashauri ya Mji wa Geita...

Michezo

Wanafunzi chuo Mwalimu Nyerere wapongezwa kwa ushindi

Spread the love  UONGOZI wa Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere (MNMA)...

Michezo

Arsenal waipopoa Manchester United

Spread the loveKLABU ya Arsenal inayoshiriki Ligi Kuu England imewatandika Mashetani Wekundu...

Michezo

Mchezaji Singida apoteza maisha mazoezini

Spread the love  MCHEZAJI na kapteni wa timu ya vijana ya Singida...

error: Content is protected !!