Tuesday , 7 May 2024
Home Habari Mchanganyiko Wana JOWUTA watakiwa kugombea uongozi, kulipa ada
Habari Mchanganyiko

Wana JOWUTA watakiwa kugombea uongozi, kulipa ada

Katibu wa JOWUTA, Selemani Msuya
Spread the love

 

WANACHAMA wa Chama cha Wafanyakazi wa Vyombo vya habari Tanzania (JOWUTA) wametakiwa kujitokeza kwa wingi kuwania nafasi za uongozi katika chama hicho huku wakisisitiziwa kulipa ada ili kuwa wagombea wenye sifa. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Rai hiyo imetolewa jana jijini Dar es Salaam na Katibu wa JOWUTA, Selemani Msuya wakati akifungua semina ya siku mbili kwa waandishi wa habari kuhusiana na mabadiliko ya tabianchi iliyoandaliwa na chama hicho chini ya ufadhili wa Shirikisho la Waandishi wa Habari Afrika (IFJ).

Msuya alisema ni muhimu kwa wanachama wa JOWUTA kuwania nafasi za uongozi katika uchaguzi unaotarajiwa kufanyika mwishoni wa mwezi Novemba huku akisisitiza ili kuweza kuwa mgombea mwenye sifa ni lazima kulipa ada.

“Kila mwanachama hai ambaye atakuwa amelipa ada anayosifa ya kuwania uongozi,  niwaombe tujitokeze kwa wingi tarehe ya uchaguzi  itakayopagwa mwezi Novemba, ili kuweza kupata viongozi bora watakaoendeleza malengo na mambo mazuri yaliyoanzishwa,” alisema Msuya na kuongeza

“JOWUTA ni taasisi iliyosajiliwa na Serikali kwa lengo la kusimamia na kushughulikia matatizo yote yanayowakumba waandishi wa habari hivyo kama viongozi tutaendelea kulisimamia jambo hilo na watakaochaguliwa watalifanyia kazi kwa nguvu zao zote suala hilo,”alisema Msuya.

Hata hivyo Msuya aliwataka waandishi wa habari waliopata fursa ya kuhudhuria mafunzo hayo kujifunza kwa kina kisha kuhabarisha watu juu ya masuala yote yanayohusiana na mabadiliko ya tabianchi.

“Chama hiki kina wanachama wengi lakini kwa siku hizi mbili za mafunzo ni waandishi wachache wamepata bahati kuhudhuria hivyo niwaombe wale wote waliopata nafasi hiyo kujifunza kwa kina na kisha kwenda kuhabarisha  na kuelimisha umma yale yote waliojifunza,” alisema Msuya

Vilevile Msuya aliishukuru IFJ kwa kufadhili mafunzo hayo kwa waandishi wa habari kutoka mikoa mitano Tanzania na kuahidi kuendelea kushirikiana nao katika kuhakikisha kundi hilo linapata mafunzo ya kutosha ya kuwajengea uwezo.

Naye Mwakilishi wa IFJ Afrika, SokhnaDia Coly alitoa wito kwa waandishi wa habari kuongeza ushirikiano ili kukuza taasisi yao.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Samia aagiza huduma za dharura maeneo yaliyoathiriwa na kimbunga Hidaya

Spread the love   RAIS wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania, Samia...

Habari Mchanganyiko

Mahakama yatoa uamuzi zuio dhidi ya Club House

Spread the loveMAHAKAMA Kuu ya Tanzania, Masjala Kuu jijini Dar es Salaam,...

Habari Mchanganyiko

GGML, OSHA yawanoa bodaboda 200 Arusha

Spread the loveZAIDI ya madereva bodaboda 200 wa jiji la Arusha wamepatiwa...

BiasharaHabari Mchanganyiko

Serikali kuwakopesha wajasiriamali 18.5bn/- kupitia NMB

Spread the loveSerikali imetenga kiasi cha Sh 18.5 bilioni kwa ajili ya...

error: Content is protected !!