Saturday , 20 April 2024
Home Habari Mchanganyiko Mfumo wa kuwanasa wezi wa machapisho waja
Habari Mchanganyiko

Mfumo wa kuwanasa wezi wa machapisho waja

Makamu mkuu wa Taasisi ya Afrika ya Sayansi na Teknologia ya Nelson Mandela (NM-AIST) Prof. Emmanuel Luoga
Spread the love

 

TAASISI ya Afrika ya Sayansi na Teknilojia ya Nelson Mandela,imefanikiwa kufanya utafiti na kuweza kugundua mfumo wa kubaini machapisho ya wizi ambao utasaidia kuwanasa baadhi ya watafiti wenye tabia ya kunakili machapisho ya watafiti wengine. Anaripoti Danson Kaijage, Dodoma … (endelea).

Hayo yameelezwa na Makamu Mkuu wa Chuo hicho Prof.Emmanuel Luoga, alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari juu ya utekelezaji na malengo ya chuo hicho katika mwaka wa fedha 2022/23.

Prof. Luoga amesema kuwa chuo hicho ambacho lengo lake ni kuwa na wanasayansi na wabunifu na kukuza teknolojia  katika nyanja mbalimbali ambazo zitasaidia kuwa na maendeleo endelevu kitaifa na kimataifa.

Pamoja na chuo hicho cha Nelson Mandela kubuni mfumo wa kubaini machapisho ya wizi ambao utaingizwa sokoni muda wowote wameanzisha kozi mbili muhimu katika chuo hicho  ambazo ni umahiri na ubunifu.

Akizungumzia dira ya chuo hicho Makamu huyo wa chuo ameeleza kuwa lengo ni kuwa taasisi ya kitaifa na kimataifa, uhandisi wa sayansi na teknolojia na ufanisi wa maendeleo endelevu na taaluma ya maendeleo ya viwanda na jamii.

Kuhusu vipaumbele amesema kuwa katika mwaka wa fedha wa mwaka 2022/23 ni kujenga mabweni ya wanawake yenye kukidhi vigezo vya akina mama wenye watoto wachanga.

Sambamba na hayo Makamu wa taasisi hiyo  ameeleza kuwa kwa kushirikiana na TARI wanafanya utafiti wa mbengu bora ya zao la Ndizi.

“Tumeisha pata aina mbili za jamii ya ndizi ambazo zinafanyiwa utafiti katika kituo cha umahiri cha utafiti wa ndizi” ameeleza Prof. Luoga.

Aidha amesema kuwa chuo hicho kitakuwa na matumizi ya TEHAMA yenye masafa marefu kwa kuimarisha mfumo huo kwa kupata ithibati kwa kiwango cha kimataifa.

Kwa upande wa msemaji wa serikali Gerson Msigwa amesema kuwa pamoja na mambo mengine amewapongeza waandishi wa habari hususani wa kitanzania kwa kuweza kuzitangaza kazi zinazofanywa na serikali.

“Napenda niwaletee salamu kutoka kwa waziri mwenye Dhamana pamoja na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hasani kwa kufanya kazi nzuri ya kutangaza kazi zinazofanywa na serikali kwa kutumia karamu zenu kizalendo.

“Kazi kubwa mnayoifanya ya kuelimisha jamii ni kazi kubwa na ya kizalendo na kwa sasa kazi kubwa ya kuelezea kazi nzuri zinazofanywa na serikali zimefanikiwa”ameeleza Msigwa.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

BiasharaHabari Mchanganyiko

Wauguzi, madaktari 1000 kugawiwa mitungi ya Oryx Gas

Spread the loveKAMPUNI ya Oryx Gas na Taasisi ya Doris Mollel Foundation...

Habari Mchanganyiko

Tanzania yachaguliwa Makamu wa Rais Tume ya Shirika la Hali ya Hewa Duniani

Spread the love  TANZANIA kupitia Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA)...

Habari Mchanganyiko

NEMC yaonya wanaojenga bila tathmini ya mazingira

Spread the loveBARAZA la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC),...

BiasharaHabari Mchanganyiko

NMB Pesa Akaunti yawavutia wakaguzi wa ndani Afrika

Spread the loveUbunifu wa bidhaa bora wa Benki ya NMB pamoja na...

error: Content is protected !!