Friday , 3 May 2024
Home Kitengo Habari Kimataifa Waziri Mkuu Uingereza amfuta kazi waziri wa fedha
Kimataifa

Waziri Mkuu Uingereza amfuta kazi waziri wa fedha

Spread the love

 

WAZIRI Mkuu wa Uingereza, Liz Truss amemfuta kazi waziri wake wa fedha, Kwasi Kwarteng, muda mfupi kabla ya kiongozi huyo kupanga kuachana na hatua za kiuchumi katika jitihada za kujinusuru na misukosuko ya kisiasa inayoikabili nchi hiyo. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea).

Truss, aliye madarakani kwa siku 37 pekee, anatathmini upya hatua za punguzo la ushuru zilizosababisha ongezeko la gharama za ukopaji na kuilazimu Benki Kuu ya Uingereza, kuingilia kati.

Aliyekuwa waziri wa mambo ya nje, Jeremy Hunt, ameteuliwa kuwa waziri mpya wa fedha kujaza nafasi ya Kwarteng.

Bado haijafahamika vipi kufutwa kazi kwa waziri huyo wa fedha kunaweza kumnusuru Truss na shinikizo kubwa dhidi yake, akilaumiwa kuwa kigeugeu kwenye utawala wake.

Liz Truss (47), aliingia madarakani miezi miwili iluyopita, baada ya Boris Johnson kulazimishwa kujiuzulu kutokana na utawala wake wa miaka mitatu kujaa misukosuko.

Kabla ya kushika madaraka ya waziri mkuu, Liz alikuwa waziri wa mambo ya nje na hivyo kuwa waziri mkuu wa nne wa Uingereza katika kipindi cha miaka sita iliyopita.

Aidha, Liz amekuwa waziri mkuu wa 15 katika kipindi cha miaka 70 aliyetwishwa jukumu la kuliongoza taifa hilo linalopitia mgogoro wa uchumi wa nishati.

 

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaKimataifa

Mwanamke Rwanda ataka kupambana tena na Kagame

Spread the loveKIONGOZI wa kihistoria wa upinzani nchini Rwanda, Victoire Ingabire Umuhoza,...

Habari MchanganyikoKimataifa

Ruto amteua Kahariri kuwa mkuu wa majeshi

Spread the loveRAIS wa Kenya, William Ruto, amemteua Jenerali Charles Muriu Kahariri,...

Habari za SiasaKimataifaTangulizi

Tanzania, Somalia kuibua maeneo mapya ya ushirikiano

Spread the love  RAIS Dk. Samia Suluhu Hassan, amesema Tanzania na Somalia...

KimataifaTangulizi

Mkuu wa majeshi Kenya afariki, Ruto atangaza maombolezo

Spread the loveRais wa Kenya, William Ruto ametangaza maombezo ya siku tatu...

error: Content is protected !!