Friday , 3 May 2024
Home Habari Mchanganyiko Majaliwa atoa wito NGO’s kufungua akaunti NMB
Habari Mchanganyiko

Majaliwa atoa wito NGO’s kufungua akaunti NMB

Spread the love

WAZIRI Mkuu Kassim Majaliwa ametoa wito kwa Mashirika yasiyo ya kiserikali (NGO’s) kufungua akaunti zao katika benki zilizopo nchini kama vile NMB ili kukuza mzunguko wa fedha na uzalendo. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea).

Majaliwa jana jijini ametoa wito huo jana tarehe 6 Oktoba jijini Dodoma wakati akizungumza na wananchi na watumishi wa Benki ya NMB alipotembelea banda la benki hiyo katika kilele cha Jukwaa la Mwaka la mashirika yasiyo ya kiserikali.

 

Meneja Mwandamizi Mahusiano Benki ya NMB, Dorah Monyo (kushoto) akitoa maelezo kwa Waziri Mkuu, Kassim majaliwa (kulia) alipotembelea banda hilo kwenye maonesho ya Jukwaa la mwaka la Mashirika yasiyo ya Kiserikali – Dodoma.

Alisema iwapo mashirika hayi yatafungua akaunti ndani ya benki ya NMB ambayo ina matawi 228 nchi nzima, mbali na kuonyesha uzalendo, lakini itasaidia kuongeza mzunguko wa fedha ndani ya nchi, jambo litakalotafsiriwa kama kitendo cha kizalendo.

Aidha, Meneja Mwandamizi wa Mahusiano wa benki ya NMB, Dorah Monyo alisema utaratibu wa kuweka fedha kwenye benki za ndani utakuwa na faida kubwa kwa wananchi kwani mzunguko wa fedha unabaki ndani.

Pia alimuahidi Waziri mkuu kuwa NMB itakuwa benki ya kwanza kusaidia mashirika hayo kuwa na akaunti ndani ya benki na zenye uendeshaji wa gharama nafuu.

Naye Mwenyekiti wa Mtandao wa Mashirika yasiyokuwa ya Kiserikali, Dk. Lilian Badi alisema ni wakati kwa taasisi binafsi kuwekeza fedha zao kwa mabenki ya nyumbani ili kuchangia ukuaji wa uchumi.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa (kulia) akijadiliana jambo na wafanyakazi wa Benki ya NMB alipotembelea banda hilo kwenye maonesho ya Jukwaa la mwaka la Mashirika yasiyo ya Kiserikali lilolofanyika Jijini Dodoma. Benki ya NMB ni mmoja wa wadau wa jukwaa hilo.

Pia, aliiomba Serikali kuzipa nafasi taasisi zisizo za kiserikali ikiwemo kuwapa uhuru wa kufanya majukumu yao kwani kwa sasa wamebanwa hasa kipengele cha usajili wa miaka 10.

Alisema kifungu hicho kinawakosesha nafasi ya kujadiliana na wadau kuhusu miradi mikubwa.

1 Comment

  • Uzalendo peke yake hautoshi. NMB inapaswa washindane na mabenki mengine yaliyoruhusiwa nchini. Kama NMB inashindwa kushindana na wenzao basi serikali itaendelea tu kutoa wito kwa NGO
    Wakati huo huo serikali iache kulazimisha mishahara na pensheni zake zipitie NMB. Waacheni wateja wajichagulie benki wazipendazo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Chadema waendelea kulilia katiba mpya

Spread the loveCHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimeendelea kudai upatikanaji wa...

BiasharaHabari Mchanganyiko

NMB yang’ara maonesho OSHA

Spread the loveBenki ya NMB imebeba tuzo ya kampuni bora kwenye sekta...

Habari MchanganyikoKimataifa

Ruto amteua Kahariri kuwa mkuu wa majeshi

Spread the loveRAIS wa Kenya, William Ruto, amemteua Jenerali Charles Muriu Kahariri,...

Habari Mchanganyiko

Chongolo aonya viongozi vijiji kutouza NIDA kwa wageni

Spread the loveMKUU wa Mkoa wa Songwe, Daniel Chongolo amewaonya viongozi wa...

error: Content is protected !!