Saturday , 20 April 2024
Spread the love

KATIKA kutekeleza mpango wa kulinda mazingirapamoja na kuunga mkono juhudi za Serikali kuifanyaTanzania kuwa nchi ya viwanda ifikapo 2025, Kampuniya Geita Gold Mining Limited (GGML) imenunua nakusimika mtambo wenye thamani ya Sh bilioni mojakwa ajili ya kuchenjua kaboni ‘makinikia’ yanayotokanana shughuli za uchimbaji wa madini ya dhahabu. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea).

Hatua hiyo inaifanya Tanzania kuwa nchi ya kwanza napekee katika ukanda wa Afrika Mashariki na Kati kuwana mtambo huo kwani hapo awali kampuni hiyo ilikuwainafuata huduma hiyo Afrika Kusini.

Hayo yamebainishwa hivi karibuni katika ziara yaWaziri wa Madini, Dotto Biteko ambaye alitembeleakampuni hiyo mkoani Geita kwa lengo la kujuamaendeleo ya GGML baada ya kuanza shughuli zauchimbaji wa chini ya ardhi katika migodi yake mitatu.

Meneja wa Idara ya Uchenjuaji, Elibariki Andrew (wa pili kutoka kushoto) akitoa maelezo kwa Waziri wa Madini,  Dk. Dotto Biteko aliyetembelea mgodi huo na kushuhudia mtambo wa uchenjuaji kaboni ulionunuliwa na kusimikwa kwa thamani ya Sh bilioni moja. Kushoto ni Mkurugenzi wa GGML, Terry Strong na Makamu Rais wa AngloGold anayeshughulikia Miradi Endelevu Ghana na Tanzania, Simon Shayo.

Akimkaribisha waziri huyo, Makamu Rais waAngloGold Ashanti anayeshughulikia Miradi endelevukwa upande wa Ghana na Tanzania, Simon Shayoalisema mradi huo utaongeza mapato kwa serikali nakampuni hiyo kwa ujumla.

“Mradi huu wa kuchenjua mabaki ya kaboniunatusaidia kuhakikisha hatuyatupi mabaki yadhahabu na mabaki yenye asili ya hewa ukaayanayoingia kwenye mazingira … kwa sababu dunianzima ipo kwenye mapambano ya kupunguza hewaukaa,” alisema.

Aidha, akizungumzia mradi huo, Dk. Biteko alisemaawali kaboni zilizokuwa zinazalishwa kwenye migodiiliyopo nchini zilikuwa zinasafirishwa kwenda nje yanchi.

“Tulizuia watu wakadhani tunafanya kitu kibaya, sasaGGML wameweka mtambo mpya ambao umegharimush bilioni moja kwa ajili kuprocess upya kaboni zadhahabu na kupata dhahabu safi badala ya kusafirishaile kaboni kupeleka nje ya nchi,” alisema.

Alisema mbali na manufaa ya mapato ambayo nchiinapata, pia watu wengi wameajiriwa kwenye mtambohuo na kuondokana na umaskini.

“Lakini pili teknolojia ya kaboni hizi ambazozinazalishwa kwenye migodi mingine zitakuwazinafanyiwa processing hapa nchini hasa ikizingatiwaile kaboni ina dhahabu.

“Mahali pengine unaweza kuona ile kaboni imetupwakama uchafu, lakini kwa taarifa tuliyopewa itazalishazaidi ya gramu 80,000, ni dhahabu nyingi zaidi ya kilo 80 kwa kaboni hii na bado itaendelea kuzalishwa maranyingi. Kwa hiyo tutapata mapato mengi zaidi,” alisemana kuongeza;  

“Hakuna mgodi mwingine ambao umetengeneza mtambo wa kuchenjua hiyo kaboni Afrika mashariki nakati kwa hiyo teknolojia hii sisi tumekuwa walimu, nawapongeza GGML kwa ubunifu huo,” alisema.

Naye Mbunge wa Geita Mjini, Constantine Kanyasu(CCM) aliipongeza kampuni hiyo kwa hatuailizochukua kuhakikisha kuwa inapanua wigo waupatikanaji wa ajira kwa Watanzania.

“Mathalani tukizungumzia local content tulitaka iwelocal of the local, nauona ushawishi huo un afanikiwakwa sababu sasa katika maeneo mengi ambayonimekwenda nimeona ushiriki wa watu wa Geita kwenye shughuli mbalimbali za uchumi wa mgodi,” alisema.

 

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

BiasharaHabari Mchanganyiko

Wauguzi, madaktari 1000 kugawiwa mitungi ya Oryx Gas

Spread the loveKAMPUNI ya Oryx Gas na Taasisi ya Doris Mollel Foundation...

Habari Mchanganyiko

Tanzania yachaguliwa Makamu wa Rais Tume ya Shirika la Hali ya Hewa Duniani

Spread the love  TANZANIA kupitia Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA)...

Habari Mchanganyiko

NEMC yaonya wanaojenga bila tathmini ya mazingira

Spread the loveBARAZA la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC),...

BiasharaHabari Mchanganyiko

NMB Pesa Akaunti yawavutia wakaguzi wa ndani Afrika

Spread the loveUbunifu wa bidhaa bora wa Benki ya NMB pamoja na...

error: Content is protected !!