RAIS wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, ametuma salamu za rambirambi kufuatia kifo cha aliyekuwa kiongozi wa kimila nchini Uingereza, Malkia Elizabeth II. Anaripoti Regina Mkonde, Dar es Salaam … (endelea).
Rais Samia ametuma salamu hizo usiku wa kuamkia leo Ijumaa, tarehe 9 Septemba 2022, ikiwa ni saa kadhaa tangu familia ya kifalme itangaze kifo hicho kilichotokea jana mchana kwenye kasri la Balmoral, nchini Scotland, ambako marehemu Malkia Elizabeth alikuwa anapatiwa matibabu.
“Nimesikitishwa na taarifa za kifo cha Malkia Elizabeth II. Kwa niaba ya Watanzania wote, natuma salamu za pole kwa Familia ya Kifalme @RoyalFamily na raia wote wa Uingereza. Malkia atakumbukwa duniani kote kama nguzo ya Amani, Umoja na Utulivu,” ameandika Rais Samia.
Nimesikitishwa na taarifa za kifo cha Malkia Elizabeth II. Kwa niaba ya Watanzania wote, natuma salamu za pole kwa Familia ya Kifalme @RoyalFamily na raia wote wa Uingereza. Malkia atakumbukwa duniani kote kama nguzo ya Amani, Umoja na Utulivu. pic.twitter.com/XsIpsYtG94
— Samia Suluhu (@SuluhuSamia) September 8, 2022
Malkia Elizabeth II aliitawala Uingereza kwa miaka 70, amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 96, ameacha watoto wanne ambao ni Prince Charles, Princess Anne, Prince Andrew na Prince Edward.
Pia, Malkia Elizabeth ameacha wajukuu nane na vitukuu 12.
Kufuatia kifo chake, mtoto mkubwa wa Malkia Elizabeth, Prince Charles anarithi mikoba yake.
Leave a comment