Friday , 29 March 2024
Home Kitengo Habari Kimataifa Jinsi mrithi wa Malkia Elizabeth anavyotawazwa kushika wadhifa huo
KimataifaTangulizi

Jinsi mrithi wa Malkia Elizabeth anavyotawazwa kushika wadhifa huo

Prince Charles
Spread the love

 

MARA tu baada ya kifo cha Malkia Elizabeth II, kiti cha ufalme kinapitishwa mara moja bila sherehe yoyote kwa mrithi wake ambaye ni mwanaye mkubwa, Charles, mkuu wa zamani wa Wales.

Lakini kuna hatua kadhaa za kiutendaji – na za kitamaduni ambazo lazima azipitie ili kutawazwa kuwa Mfalme.

Ataitwa nani?
Moja kati ya vitu vya kwanza atakavyofanya ni kuamua kama atatawala kama Mfalme Charles III, au kuchukua jina lingine.

Kwa mfano, jina la babu yake George VI lilikuwa Albert, lakini alitawala kwa kutumia mojawapo ya majina yake ya kati.

Charles anaweza kuchagua kutoka kwa mojawapo ya majina yake manne – Charles Philip Arthur George.

Sio yeye pekee ambaye anakabiliwa na kubadilisha jina lake.

Ingawa yeye ndiye mrithi wa kiti cha ufalme, Prince William hatakuwa Mkuu wa Wales moja kwa moja.

Hata hivyo, moja kwa moja anarithi jina lingine la baba yake, Duke of Cornwall.

Mkewe Catherine atajulikana kama Duchess of Cornwall.

Pia kutakuwa na jina jipya la mke wa Charles, ambaye majina yake kamili yatakuwa Malkia Consort – neno linalotumiwa kwa mwenzi wa mfalme.

Sherehe rasmi
Katika muda wa saa 24 au zaidi baada ya kifo cha mamake, Charles atatangazwa rasmi kuwa Mfalme.

Hii itafanyika katika kasri la St James’s huko London, mbele ya baraza la sherehe linalojulikana kama Baraza la kukabidhi Mamlaka.

Hii inaundwa na wajumbe wa Baraza la Siri – kikundi cha Wabunge wakuu, wa zamani na wa sasa, na wenzao – pamoja na baadhi ya watumishi waandamizi wa serikali, makamishna wakuu wa Jumuiya ya Madola, na Meya wa London.

Zaidi ya watu 700 wana haki ya kuhudhuria, lakini kutokana na ilani hiyo fupi, huenda idadi halisi ikawa ndogo sana.

Katika Baraza la kukabidhi Mamlaka mnamo 1952, karibu watu 200 walihudhuria. Kiutamaduni, Mfalme hahudhurii.

Katika mkutano huo, kifo cha Malkia Elizabeth kitatangazwa na Rais wa Baraza la Siri (kwa sasa akiwa ni Penny Mordaunt Mbunge), na tangazo litasomwa kwa sauti.

Maneno ya tangazo hilo yanaweza kubadilika, lakini kiutamaduni imekuwa mfululizo wa sala na ahadi, kumpongeza mfalme aliyetangulia na kuahidi kumuunga mkono mfalme mpya.

Malkia Elizabeth II

Tangazo hili kisha linatiwa saini na watu kadhaa wakuu akiwemo waziri mkuu, Askofu Mkuu wa Canterbury, na Bwana Chansela.

Kama ilivyo kwa sherehe hizi zote, tahadhari itakuwa kwa kile ambacho kinaweza kuwa kimebadilishwa, kuongezwa au kusasishwa, kama ishara ya enzi mpya.

Tangazo la kwanza la Mfalme
Baraza la kukabidhi Mamlaka hukutana tena – kwa kawaida siku moja baadaye – na wakati huu, Mfalme atahudhuria, pamoja na Baraza la Siri.

Hakuna ”Kuapishwa” mwanzoni mwa utawala wa mfalme wa Uingereza, kwa mtindo wa wakuu wengine wa nchi, kama vile Rais wa Marekani.

Lakini kuna tamko lililotolewa na Mfalme mpya na – kulingana na mila ya mwanzoni mwa Karne ya 18 – atakula kiapo cha kuhifadhi Kanisa la Scotland.

Baada ya mbwembwe za wapiga tarumbeta, tangazo la umma litatangazwa kumtangaza Charles kama Mfalme mpya.

Hii itafanywa kwenye roshani juu ya Mahakama ya Friary katika eneo la Kifalme la St James, na afisa anayejulikana kama Garter King of Arms.

Malkia Elizabeth II alimtawaza mtoto wake Charles kama Prince of Wales mnamo 1969
Atasema: ”Mungu mwokoe Mfalme”, na kwa mara ya kwanza tangu 1952, wimbo wa taifa utakapopigwa maneno yatakuwa ”Mungu Mwokoe Mfalme”.

Risasi zitapigwa katika eneo la Hyde Park, Mnara wa London na kutoka kwa meli za wanajeshi wa majini, na tangazo la kumtangaza Charles kama Mfalme litasomwa huko Edinburgh, Cardiff na Belfast.

Kutawazwa
Ishara ya juu ya kukabidhi mamlaka itakuwa kutawazwa, wakati Charles atavikwa taji rasmi.

Kwa sababu ya maandalizi yanayohitajika, kutawazwa hakuwezi kutokea mara tu baada ya Charles kukabidhiwa madaraka – Malkia Elizabeth alirithi kiti cha enzi mnamo Februari 1952, lakini hakutawazwa hadi Juni 1953.

Kwa miaka 900 iliyopita kutawazwa kumefanyika Westminster Abbey – William the Conqueror alikuwa mfalme wa kwanza kutawazwa huko, na Charles atakuwa wa 40.

Ni huduma ya kidini ya Kianglikana, inayofanywa na Askofu Mkuu wa Canterbury.

Katika kilele cha sherehe hiyo, ataweka Taji la St Edward juu ya kichwa cha Charles – taji thabiti la dhahabu, lililoanzia 1661. Hiki ndicho kitovu cha Vito vya Taji kwenye Mnara wa London, na kwa sasa huvaliwa tu na mfalme wakati wa kutawazwa kwenyewe (kwa sababu lina uzito mkubwa wa 2.23kg).

Tofauti na harusi za kifalme, kutawazwa ni tukio rasmi la serikali – serikali inalipa, na hatimaye huamua orodha ya wageni.

Kutakuwa na muziki, usomaji na ibada ya kumtia mafuta mfalme mpya, kwa kutumia mafuta ya machungwa, waridi, mdalasini, miski na ambari.

Mfalme mpya atakula kiapo cha kutawazwa mbele ya ulimwengu watu wakiwa wanatazama.

Wakati wa sherehe hii, atapokea taji umbo la duara na fimbo kama ishara ya jukumu lake jipya na Askofu Mkuu wa Canterbury ataweka taji imara la dhahabu juu ya kichwa chake.

Mkuu wa Jumuiya ya Madola
Charles amekuwa mkuu wa Jumuiya ya Madola, chama cha nchi huru 56 na watu bilioni 2.4.

Kwa nchi 14 kati ya hizi, pamoja na Uingereza, Mfalme ndiye mkuu wa nchi.

Nchi hizi zinazojulikana kwa jina la Jumuiya ya Madola ni: Australia, Antigua and Barbuda, Bahamas, Belize, Canada, Grenada, Jamaica, Papua New Guinea, St Christopher na Nevis, St Lucia, St Vincent and Grenadines, New Zealand, Solomon. (CHANZO BBC)

1 Comment

  • Je wangapi wanajua kuwa wananchi WENGI wa Uingereza hawataki kutawaliwa na mfalme?
    Soma magazeti ya huko yaitayo the Guardian, National, Reuter,s Herald Scotland na kadhalika
    Badala ya kufuata na kurudia propaganda za BBC, Sky, CNN etc

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoKimataifa

Zuma akataliwa kugombea urais

Spread the loveTUME Huru ya Uchaguzi Afrika Kusini (IEC) imemwondoa rais wa...

KimataifaTangulizi

Zuma akataliwa kugombea urais

Spread the love  TUME Huru ya Uchaguzi Afrika Kusini (IEC) imemwondoa rais...

Habari za SiasaTangulizi

CAG: Wastaafu, wenza wao chanzo NHIF kufilisika

Spread the loveRIPOTI ya ukaguzi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu...

Habari za SiasaTangulizi

Vikundi hewa 851 vyalamba bilioni 2.6 mikopo ya halmashauri

Spread the loveVIKUNDI hewa vya wajasirimali wadogo 851 kutoka katika halmashauri 19...

error: Content is protected !!