Saturday , 27 April 2024
Home Kitengo Habari Kimataifa Prof. Wajackoyah afanikiwa kupiga kura baada ya kusubirishwa kwa saa tatu
Kimataifa

Prof. Wajackoyah afanikiwa kupiga kura baada ya kusubirishwa kwa saa tatu

Profesa George Wajackoyah
Spread the love

 

HATIMAYE Mgombea Urais wa chama cha Roots Party of Kenya, Prof. George Wajackoyah,amefanikiwa kupiga kura baada ya kuchelewa kwa saa tatu kutokana na vifaa vya kielekroniki vya kutambua wapiga kura (KIEMS) kushindwa kumtambua. Anaripoti Apaikunda Mosha, TUDARCo … (endelea).

Prof. Wajackoyah leo Jumanne tarehe 9 Agosti, 2022, amewasili shule ya msingi Indangalasia majira ya saa 4:15 katika kaunti ya Kamega.

Alifanikiwa kuanza kupiga kura yake saa 7.00 mchana baada ya bodi ya kusimamia uchaguzi kumruhusu kupiga kura kwa kutumia daftari la wapiga kura.

Mbio za urais zimewavutia washindani wanne Prof. Wajackoyah, David Mwaure wa chama cha Agano, Naibu Rais William Ruto wa Kenya Kwanza na Azimio la umoja Raila Odinga.

Vituo vya upigaji kura vilifunguliwa saa 12 asubuhi nchi nzima, DP Ruto na Mwaure walikuwa miongoni mwa wagombea waliowahi kupiga kura.

Dk. Ruto alipiga kura dakika chache kufikia saa 12 asubuhi katika shule ya Msingi ya Kosachei huko Sugoi, akiambatana na mkewe Mama Rachel Ruto.

Mwaure amepiga kura katika shule ya Sekondari Upper hill huko Nairobi akiwa na mke wake Anna Mwaure majira ya saaa 1:15 asubuhi.

Wapinzani wenzao, makamu wa Rais wa zamani Raila Odinga alitarajia kupiga kura katika shule ya Msingi Old Kibera huko Nairobi.

Wananchi 22,120,458 waliosajiliwa kupiga kura wataenda kupiga kura mwaka huu ili kuchagua wajumbe 290 wa bunge la Taifa, wajumbe 1,450 wa bunge la kaunti, magavana 47 na wawakilishi, viongozi wa wanawake pamoja na mrithi wa Rais Uhuru Kenyatta.

Uchaguzi unajumuisha vyama 63 vya siasa, angalau na wagombea 11,330 wakigombania nafasi tofauti tofauti.

Mashindano makubwa ya kisiasa pia yamevutia wagombea binafsi 3,752 kuwania nafasi tofauti tofauti ndani ya nchi .

Kwa mujibu wa IEBC taarifa za uchaguzi, wanawake 261 wamegombea nafasi ya MP nchini , wakati watu 1,473 wamegombea nafasi za Ubunge.

Wagombea wengine wakiwemo watu 9,142 ambao wanagombea nafasi za Bunge la kaunti, wakati watu 183 na 263 wanagombea kuwa magavana na seneta mtawalia.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaKimataifaTangulizi

Tanzania, Somalia kuibua maeneo mapya ya ushirikiano

Spread the love  RAIS Dk. Samia Suluhu Hassan, amesema Tanzania na Somalia...

KimataifaTangulizi

Mkuu wa majeshi Kenya afariki, Ruto atangaza maombolezo

Spread the loveRais wa Kenya, William Ruto ametangaza maombezo ya siku tatu...

Kimataifa

Majaji kuamua hatima ya Zuma leo

Spread the loveMajaji nchini Afrika Kusini leo Jumanne wataamua ikiwa rais wa...

Habari za SiasaKimataifa

Spika Afrika Kusini ajiuzulu kwa tuhuma za rushwa

Spread the loveSpika wa Bunge la Afrika Kusini, Nosiviwe Mapisa-Nqakula ametangaza kujiuzulu...

error: Content is protected !!