Friday , 10 May 2024
Home Kitengo Habari Kimataifa Waandamana kumpinga Rais kisa ongezeko gharama za maisha, rushwa Afrika Kusini
Kimataifa

Waandamana kumpinga Rais kisa ongezeko gharama za maisha, rushwa Afrika Kusini

Spread the love

 

WAANDAMANAJI takribani 300, ambao ni wanachama wa chama tawala cha ANC cha Afrika Kusini, wametinga makao makuu ya chama hicho jijini Johannesburg , wakishinikiza Rais wa Taifa hilo, Cyril Ramaphosa ajiuzulu, wakidai ameshindwa kudhibiti ongezeko la gharama za maisha. Inaripoti Mitandao ya Kimataifa … (endelea).

Kwa mujibu wa mtandao wa Aljazeera, wanachama hao wa ANC, waliandamana jana Ijumaa, tarehe 15 Julai 2022, wakimtaka Rais Ramaphosa ajiuzulu.

Mbali na sbaabu ya ongezeko la gharama za maisha, waandamanaji hao wanamtaka Rais Ramaphosa ajiuzulu, wakimtuhumu ameshindwa kudhibiti ongezeko la bei ya mafuta, changamoto ya kukatika kwa umeme na kukithiri kwa rushwa kwenye taasisi za umma.

Mratibu wa maandamano hayo, Carl Niehaus, ambaye ni mwanachama mwandamizi wa ANC, amesema hatua hiyo inalenga kufikisha huzuni ya wananchi dhidi ya Rais Ramaphosa, aliyedai kuwa ameshindwa kuiongoza nchi.

Hata hivyo, Rais Ramaphosa amenukuliwa na vyombo vya habari akikanusha tuhuma hizo, huku akisema hatatishika na mashinikizo yanayotolewa dhidi yake.

1 Comment

  • Mandela kazi ilimshinda, Zuma kazi ilimshinda, na sasa kazi inakushinda. Acheni kuongoza kwa mazoea. Viongozi hawa wote wameshindwa kuwakomboa weusi wanaowaongoza!

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaKimataifa

Israel yatia shubiri Gaza wakisherehekea Hamas kusitisha mapigano

Spread the loveWAKATI kundi la Hamas huko Gaza likitangaza kuridhia pendekezo lao...

KimataifaMakala & Uchambuzi

Mbivu, mbichi urais wa Ramaphosa mwezi huu

Spread the loveMWISHONI mwa mwezi huu, raia wa Afrika Kusini watapiga kura...

Habari za SiasaKimataifa

Mwanamke Rwanda ataka kupambana tena na Kagame

Spread the loveKIONGOZI wa kihistoria wa upinzani nchini Rwanda, Victoire Ingabire Umuhoza,...

Habari MchanganyikoKimataifa

Ruto amteua Kahariri kuwa mkuu wa majeshi

Spread the loveRAIS wa Kenya, William Ruto, amemteua Jenerali Charles Muriu Kahariri,...

error: Content is protected !!