Thursday , 2 May 2024
Home Habari Mchanganyiko Uamuzi kesi ya kina Mdee leo
Habari MchanganyikoTangulizi

Uamuzi kesi ya kina Mdee leo

Spread the love

MAHAKAMA Kuu ya Tanzania, Masjala Kuu ya Dar es Salaam, inatarajia kutoa uamuzi dhidi ya maombi yaliyofunguliwa na wabunge viti maalum 19, wakiongozwa na Halima Mdee, ya kuomba kibali cha kufungua kesi ya kupinga kuvuliwa uanachama wa chama cha Chadema. Anaripoti Regina Mkonde, Dar es Salaam…(endelea).

Uamuzi huo unatarajiwa kutolewa leo Ijumaa, tarehe Julai 202, mahakamani hapo mbele ya Jaji Mustafa Ismail.

Mahakama hiyo inatarajiwa kutoa uamuzi kama inatoa kibali cha kufunguliwa kesi hiyo  ya kina Mdee kupinga kuvuliwa uanachama wa Chadema, au la.

Uamuzi huo ulikuwa utolewe juzi Jumatano tarehe 6 Julai, 2022, lakini ilishindikana baada ya mahakama kusema bado haujakamilika.

Mdee na wenzake wanadai, mchakato wa kuwafukuza uanachama ulikuwa kinyume cha Katiba ya Chadema na Katiba ya nchi.

Miongoni mwa hoja hizo Tano ni, maombi ya kuomba mapitio hayo yalifunguliwa ndani ya muda kisheria, wabunge hao kuwa na maslahi dhidi ya mchakato huo wakidai uliwaathiri kufuatia hatua ya Chadema kuwavua uanachama.

Nyingine ni, mchakato huo kuingiliwa na upendeleo kufuatia ya wajumbe wa Kamati Kuu ya Chadema, waliowafukuza uanachama, kushiriki kikao Cha Baraza Kuu la Chadema, kilichotupilia mbali rufaa zao za kupinga kufukuzwa.

Hoja nyingine ni maamuzi ya Chadema kuwafukuza uanachama kuwa ya umma na mwisho ikiwa wabunge hao kukosa nafasi ya kupata haki Yao ya kusikilizwa juu ya uamuzi huo.

Mbali na Chadema iliyoshtakiwa kupitia Bodi yake ya Wadhamini, wajibu maombi wengine katika shauri hilo ni, Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) na Mwansheria Mkuu wa Serikali (AG).

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Chadema waendelea kulilia katiba mpya

Spread the loveCHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimeendelea kudai upatikanaji wa...

Habari za SiasaTangulizi

Chadema kumshtaki Rais Samia

Spread the loveCHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimetishia kumfungulia kesi ya...

BiasharaHabari Mchanganyiko

NMB yang’ara maonesho OSHA

Spread the loveBenki ya NMB imebeba tuzo ya kampuni bora kwenye sekta...

Habari MchanganyikoKimataifa

Ruto amteua Kahariri kuwa mkuu wa majeshi

Spread the loveRAIS wa Kenya, William Ruto, amemteua Jenerali Charles Muriu Kahariri,...

error: Content is protected !!