
Klabu ya soka ya Yanga Mabigwa wa Ligi ya NBC usiku wa jana 7 julai 2022 wameibuka vinara baada ya kutwaa tuzo nyingi katika hafla ya usiku wa mastaa wa soka iliyofanyika kwenye ukumbi wa Johari Rotana Hotel jijini Dar es salaam na kuhudhuriwa na wadau mbalimbali wa Soka. Anaripoti Damas Ndelema Tudarco endelea
Katika hafla ya usiku wa Mastaa wa Soka klabu ya Yanga ilifanikiwa kubeba tuzo 14, ukilinganisha na klabu zingine amabapo klabu hiyo ilifanikiwa kupata tuzo za mshindi wa Ligi ya NBC na mshindi wa Azam Sports Federation na zingine zikiwa za wachezaji na makocha
Tuzo ambazo zilibebwa na wachezaji wa Yanga na makocha ni pamoja na Mchezaji bora wa Msimu na kiungo bora wa Msimu zilienda kwa Yannick Bangala raia wa kongo, kipa bora wa msimu ilienda kwa Djigui Diarra amabaye pia alifanikiwa kupata tuzo ya mchezaji mwenyewe fair play.
Tuzo ya goli bora la msimu ilibebwa na Fiston Mayele goli lake la Acrobatic dhidi ya Biashara united, tuzo ya kocha bora wa msimu ilienda kwa Nasreddine Nabi ambae aliingoza Yanga kutwaa ubigwa pasipo kupoteza mchezo wowote ule
Aidha tuzo zingine ni tuzo ya mchezaji bora chipukizi kwa upande wa wanawake ambayo ilichukuliwa na mchezaji wa Yanga princess Clara Luvanga
Pia Yanga walifanikiwa kuingiza wachezaji sita katika kikosi bora cha msimu wa 2021/22 , wachezaji hao ni pamoja na Dijgui Diarra, Djuma Shaban, Bakari Mwamunyeto, Yannic Bangala, Feisal Salam na Fiston Mayele
More Stories
Ligi Kuu kuanza kutimua vumbi leo
Yanga yairarua Simba, Mayele atetema
Tume ya Ajira yataja sababu vijana kukosa ajira