Sunday , 5 May 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Mbunge alia ukata balozi za Tanzania
Habari za Siasa

Mbunge alia ukata balozi za Tanzania

Mbunge wa Bunge la Tanzania, Felister Njau
Spread the love

 

MBUNGE wa Bunge la Tanzania, Felister Njau, ameeleza kusikitishwa na kitendo cha Serikali kushindwa kutoa fedha zinazopangwa kupelekwa kwenye balozi za Tanzania katika nchi mbalimbali. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dodoma … (endelea).

Mbunge huyo ameeleza hayo leo Ijumaa tarehe 17 Juni, 2022, wakati akichangia hoja ya bajeti ya Seriklai bungeni jijini Dodoma.

Njau amesema kuna balozi sita zilishindwa kutekeleza diplomasia ya uchumi kwa vitendoe kwa kutopelekwa kwa fedha zilizopangwa katika mwaka wa fedha 2020/21.

Amesema katika mwaka huo wa fedha Sh 116 milioni zilipangwa kupelekwa ubalozi wa Tanzania DRC lakini zilipelekwa 13 milioni sawa na asilimia 11.

Pia alisema ubalozi wa Lilongwe nchi Malawi ulitengewa Sh 57 milioni lakini zilizopelekwa ni Sh12 milioni, “tunaingiaje kwenye ushindani wa kiuchumi kama reception zetu hazipo vizuri,” amesema Njau.

Ameongeza kuwa ubalozi wa Ethiopia ulitengewa Sh138 milioni lakini zimepelekwa Sh2 milioni tu huku ubalozi wa Washington DC nchini Marekani ukitengewa Sh144 milioni lakini zilipelekwa Sh8 milioni tu sawa na asilimia saba, “how can we move kama nchi kama tunafanya mambo haya.”

Pia amesema watumishi wa balozi licha ya kubeba mzigo kwa kuwa pungufu lakini wamekuwa wakidai malimbikizo ikiwemo ubalozi wa Tanzania nchini Ufaransa, Malysia, DRC na Afrika Kusini.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaTangulizi

Mbatia ambwaga Selasini, mahakama yaamuru alipwe fidia

Spread the loveMAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu, jijini Dar es Salaam, imemuamuru...

Habari za SiasaTangulizi

Mkulo afariki dunia, kuzikwa kesho Kilosa

Spread the loveALIYEKUWA Waziri wa Fedha na Mbunge wa Kilosa (CCM), Mustafa...

Habari za SiasaTangulizi

Sabaya afutiwa kesi, ruksa kugombea uongozi

Spread the loveMwendesha Mashtaka Mkuu wa Serikali DPP leo Ijumaa amefuta rufaa...

Habari za Siasa

Serikali yasaka bilioni 3 kujenga daraja Mto Mpiji

Spread the loveSerikali imesema inaendelea na juhudi za kutafuta fedha kiasi cha...

error: Content is protected !!