Monday , 6 May 2024
Home Gazeti Habari Rasmi Pogba aondoka Manchester United
HabariMichezo

Rasmi Pogba aondoka Manchester United

Spread the love

 

KLABU ya Manchester United imeachana rasmi na kiungo wake Paul Pogba, mara baada ya kumaliza mkataba wake ndani ya klabu hiyo ambayo amehudumu kwa nyakati tofauti toka mwaka 2012. Anaripoti Kelvin Mwaipungu…(endelea)

Kiungo huyo raia wa Ufaransa mwenye taji la kombe la Dunia, anaachana na Manchester United kama mchezaji huru kufuatia kugoma kuongeza mkataba mpya siku za hivi karibuni.

Pogba ambaye amekulia kwenye klabu hiyo kwenye maisha yake ya soka, aliondoka kwa mara ya kwanza msimu wa 2012 na kujiunga na klabu ya Juventus ya Itary ambapo alihudumu kwenye msimu minne kisha 2016, alirejea tena Manchester United chini ya Jose Mourinho.

Kurejea mchezaji huyo nadni ya Manchester United, kulimfanya kuwa mchezaji ghali wakati huyo kufuatia uhamisho wake kuwa wa bei kubwa, kiasi kilichowalazimu mashetani wekundu hao kutoa kitita cha Pauni Milioni 89.

Kwenye msimu uliomalizika Pogba amecheza jumla ya michezo 27, huku klabu yake ya Manchester United ikimaliza kwenye nafasi ya sita, na kushindwa kufuzu kucheza michuano ya Ligi ya Mabingwa Barani Ulaya.

Katika kipindi chote cha miaka sita ndani ya klabu ya Manchester United, Pogba alicheza jumla ya michezo 226 na kupachika mabao 39.

Mchezaji huyo anaondoka ndani ya Manchester United, huku ikiwa bado haijafahamaika ankwenda wapi lakini vyanzo vingi vya taarifa Barani Ulaya, vikieleza kuwa huwenda mchezaji huyo akarudi Juventus.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Michezo

Ligi mbalimbali za pesa kuendelea leo

Spread the love JUMAPILI ya leo imekaa kipesa tuu yani baada ya...

Michezo

Usiishie kuangalia tu game za leo, piga na mkwanja na Meridianbet

Spread the love  LIGI mbalimbali barani ulaya zitarejea tena Jumamosi ya leo...

Michezo

Ligi mbalimbali za pesa kuendelea leo

Spread the love Ijumaa ya leo ambapo mechi mbalimbali zinaendelea Duniani Meridianbet...

Michezo

Europa na Conference kukupatia pesa ndefu leo

Spread the love  ALHAMISI ya leo tutaenda kushuhudia mitanange ya kukata na...

error: Content is protected !!