Friday , 3 February 2023
Home Gazeti Habari za Siasa Mradi wa Umeme Rufiji kutumia asilimia 51 ya bajeti nzima ya Nishati
Habari za Siasa

Mradi wa Umeme Rufiji kutumia asilimia 51 ya bajeti nzima ya Nishati

Bwawa la Umeme Rufiji
Spread the love

SERIKALI imetenga Sh 1.44 trilioni katika mwaka wa fedha 2022/23 kwaajili ya kutekeleza kazi mbalimbali kwenye mradiMradi wa Kuzalisha Umeme kwa Kutumia Maji wa Julius Nyerere (JNHPP). Anaripoti Mwandishi Wetu, Dodoma … (endelea).

Kiasi hicho ni sawa na asilimia 51 ya Sh 2.7 trilioni iliyopangwa kwa bajeti nzima ya Wizara ya Nishati kwa mwaka wa fedha 2022/23.

Mradi huo unaotarajiwa kuchangia MW 2,115 katika Gridi ya Taifa baada ya kukamilika, unagharimu Sh 6.55 trilioni na unatarajiwa kuimarisha upatikanaji wa umeme wa uhakika nchini.

Akiwasilisha bungeni makadirio ya mapato na matumizi kwa mwaka 2022/23, Waziri wa Nishati, Januari Makamba amesema pamoja na kazi nyingine za kiufundi zilizopangwa kufanywa, katika mwaka ujao wa fedha Serikali itaongeza umahiri na weledi kwenye usimamizi wa mradi.

Amesema lengo ni kuhakikisha, “kwamba unamalizika ukiwa katika usalama na viwango stahili na malengo yake yanatimia.”

Kwa mujibu wa Ripoti ya CAG yam waka 2020/21 hadi kufikia tarehe 31 Oktoba 2021, utekelezaji wa mradi huo ulikuwa umefika asilimia 48.02 tu badala ya asilimia 94.47 iliyokuwa imepangwa.
Hali hiyo inaonesha kuwa mradi ulikuwa umechelewa kwa asilimia 46.45 kama ilivyooneshwa kwenye mpangokazi.

Aidha, Taarifa ya Maendeleo ya Mradi ya Tarehe 31 Oktoba 2021 ilionesha kuwa mradi ulikuwa umechelewa kukamilika kwa muda wa siku 477.

Taarifa hiyo ya maendeleo ya mradi ilieleza kuwa sababu ya mradi kuchelewa ni kuchelewa kuwasilishwa na kuidhinishwa kwa usanifu wa mwisho wa mradi, janga la mafuriko kwenye Mto Rufiji, pamoja Janga la UVIKO-19. Ucheleweshaji huu unaweza kusababisha kuongezwa kwa muda wa utekelezaji wa mradi hivyo kuhitaji fedha za ziada za kugharamia shughuli za wakandarasi na washauri juu ya usimamizi wa mradi.

January Makamba, Waziri wa Nishati

Aidha, CAG aibaini kuwa ingawa hadi tarehe 31 Oktoba 2021 hakukuwa na mpangokazi uliofanyiwa mapitio na marekebisho, mkandarasi alikuwa tayari ametumia miezi 34 na nusu kutekeleza asilimia 48.02 ya kazi huku kazi ikiwa imepangwa kukamilika ndani ya miezi 42.

Kwa mujibu wa CAG hadi tarehe 31 Oktoba 2021, mkandarasi alikuwa amebakiwa na muda wa miezi sita na nusu kukamilisha kazi hiyo kwa mujibu wa mpangokazi kwani mradi unatarajiwa kukamilika tarehe 14 Juni 2022.

“Kukosekana kwa mpangokazi uliorekebishwa kunaweza usababisha madai yasiyotarajiwa kutokana na usimamizi duni wa mkataba hivyo kuchelewesha kukamilisha mradi kwa kukosekana mpango halisi wa kupima na kufuatilia maendeleo ya mradi kwa hatua na wakati stahiki,” amesema CAG katika ripoti yake.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Vijana ACT-Wazalendo Dar wampa tano Rais Samia

Spread the love  NGOME ya Vijana ya Chama cha ACT-Wazalendo, kimempongeza Rais...

Habari za Siasa

ACT-Wazalendo yaiangukia Serikali kunusuru wananchi Liwale, Nachingwea

Spread the love  CHAMA cha ACT-Wazalendo, kimeitaka Serikali kuchukua hatua za haraka...

Habari za SiasaTangulizi

Vigogo wanaokwamisha mradi Liganga na Mchuchuma kitanzani

Spread the love  NAIBU Spika wa Bunge, Mussa Zungu, watu wanaokwamisha utekelezaji...

Habari za Siasa

Gridi ya Taifa kufumuliwa kukabiliana na katizo la mgao wa umeme

Spread the love  WAZIRI wa Nishati, Januari Makamba, amesema Serikali ina mpango...

error: Content is protected !!