Wednesday , 8 May 2024
Home Habari Mchanganyiko NMB yawaita wafanyabiashara kuchangamkia fursa miradi ya kimkakati
Habari Mchanganyiko

NMB yawaita wafanyabiashara kuchangamkia fursa miradi ya kimkakati

Spread the love

BENKI ya NMB nchini Tanzania imesema ipo tayari kutoa fedha kuwezesha wafanyabisahara wakubwa, wakati na wadogo kuchangamkia fursa kwenye miradi mbalimbali ya kimkakati ikiwemo miradi wa bomba la mafuta na ujenzi wa reli wa (SGR) ili kuchangia maendeleo ya Taifa hilo. Anaripoti Mwandishi Wetu…(endelea).

Mkuu wa Kitengo cha miamala wa Benki ya NMB, Linda Teggisa, akizungumza wakati wa hafla fupi iliyo kutanisha wadau wa Mafuta na Gesi na kufanya majadiliano, iliyofanyika katika Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam jana ambapo Benki ya NMB ilikuwa ni miongoni mwa wadhamini.

Kwa mujibu wa Mkuu wa Kitengo cha Mifumo ya Miamala wa Benki ya NMB, Linda Teggisa, amesema benki yake inatoa hadi Sh.326 bilioni (sawa na dola milioni 140) kwa mkopaji mmoja.

Meneja Mwandamizi wa Kitengo cha Biashara wa Benki ya NMB, Christopher Mgani, akifafanua jambo kwa wadau kuhusu Bidhaa za Benki hiyo wakati wa hafla fupi iliyokutanisha wadau wa Mafuta na Gesi na kufanya majadiliano, iliyofanyika katika Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam jana ambapo Benki ya NMB ilikuwa ni miongoni mwa wadhamini.

Akizungumza katika hafla ya jioni iliyoandali wa mwamvuli wa Watoa Huduma kwenye Sekta ya Mafuta na Gesi (ATOGS) jijini Dar es Salaam ljumaa ya tarehe 27 Mei 2022, Teggisa alisema NMB inatambua mahitaji ya wafanyabiashara wanaoshiriki katika utekelezaji wa miradi ya kimkakati na ndio maana ilikuja na suluhishi mahususi zinazolenga mahitaji yao na mnyororo wa kuongeza thamani kama usafiri, bima na uzalishaji.

“Benki ya NMB imejipanga kutoa mchango mkubwa wa kifedha kuwawezesha wafanyabiashara wakubwa, wa kati na wadogo ili waweze kuchangamkia fursa mbalimbali kwenye miradi ya kimkakati na sekta ya nishati, mafuta na gesi. Kama benki, nia yetu ni kuhakikisha kuwa Watanzania wanashiriki kikamilifu bila vikwazo vya fedha,” alisema.

Teggisa alisema hadi mwezi huu, benki yake imetoa kiasi cha bilioni 469.9 kama mikopo kwa wadau mbalimbali kwenye sekta ya mafuta na gesi.

“Tutaendelea kotoa huduma za kibenki zinazoendana na mahitaji ya soko la sasa katika harakati zetu za kuchangia maendeleo ya taifa letu. Pia tumeweza kuja na mifumo inayowezesha malipo ya serikali kupitia mfumo wa GePG ili kuwezesha malipo ya kodi na huduma mbalimbali ya serikali.

Baadhi ya Viongozi wa Benki ya NMB wakiwa katika picha ya pamoja na wadhamini wenzao katika hafla ya Mafuta na Gesi baada ya kumalizika majadiliano hayo yaliyofanyika katika Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam.

Kwa upande wake, Meneja Mwandamizi wa Kitengo cha Biashara, Christopher Mgani aliwasihi wafanyabisahara nchini kuchangamkia fursa ya Bancassurance inayotolewa na benki hiyo ili kupunguza hatari kwenye biashara zao.

“Kupitia huduma yetu ya Bancassurance, mfanyabiashara atafanya biashara yake kwa uhuru kwa kuwa huduma hii inampatia bima ya kujikinga na majanga mbalimbali ikiwemo uharibifu wa mali, afya na tayari tumejiunga na makampuni 10 nchini kutoa huduma hii nchi nzima,” alisema.

Naye mwenyekiti wa Bodi ya ATOG, Abdulsamad Abdulrahim aliishukuru benki ya NMB kwa uzalendo kwa jitihada zake za kuchangia miradi mbalimbali ya kimkakati, nishati, mafuta na gesi.

“Tunaishukuru benki ya NMB kwa kuja na huduma za kibenki zinazolenga kusaidia wafanyabiashara mbalimbali. Benki hii imeenda mbali kwa kurekebisha masharti hasa kwenye upande wa dhamana . Hiki kilikuwa kilio cha wafanyabiashara wengi kwa miaka mingi na tunaishukuru benki kwa kuona mbali na kilifanyia kazi jambo hili,” alisema.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

BiasharaHabari Mchanganyiko

NBC, SILABU waungana kufikisha elimu ya fedha majumbani

Spread the loveBenki ya Taifa ya Biashara (NBC) imeingia makubaliano ya ushirikiano...

AfyaHabari MchanganyikoMakala & Uchambuzi

Kisukari cha mimba ni nini?

Spread the loveKisukari cha mimba ni aina ya kisukari kinachotokea kwa baadhi...

Habari Mchanganyiko

Mafunzo kwa bodaboda 395 yamkuna Meya Dodoma

Spread the loveNAIBU Meya wa Jiji la Dodoma, Asma Karama amepongeza mafunzo...

Habari Mchanganyiko

Samia aagiza huduma za dharura maeneo yaliyoathiriwa na kimbunga Hidaya

Spread the love   RAIS wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania, Samia...

error: Content is protected !!