Spread the love

SOKO la Vetenari, lililoko wilayani Temeke, Mkoa wa Dar es Salaam, limeteketea kwa moto usiku wa kuamkia leo Jumatatu, huku taarifa za awali zikidai chanzo chake ni hitilafu ya umeme. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam…(endelea).

Akizungumza na wafanyabiashara baada ya kutembelea soko hilo, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, takribani vibanda 453 vimeteketea na kuathiri wafanyabiashara zaidi ya 800.

“Niungane na wenzangu kutoa pole kwa wafanyabiashara wote wa soko hili, mimi alfajiri Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaa, ACP Jumanne Muliro amenipigia siku kwamba tupo tunazima moto. Moto umewaathiri wafanyabiashara 803 na kuteketekeza vibanda 453. Hili ni pigo kubwa kiuchumi,” amesema Makalla.

Mkuu huyo wa Mkoa wa Dar es Salaam, amesema Serikali itachukua jitihada za haraka kulikarabati soko hilo, wafanyabiashara waendelee na shughuli zao.

Aidha, amepiga marufuku shughuli za uunganishaji umeme kiholela pamoja na mamantilie kupika wakati wa usiku ambapo watu wanakuwa hawapo sokoni.

Mkuu wa Wilaya ya Temeke, Jokate Mwegelo, amesema watazitumia Sh. 400 milioni, fedha zilizotolewa na Rais Samia Suluhu Hassan, kwa ajili ya kuboresha shughuli za wafanyabiashara wadogo ‘wamachinga’, kukarabati soko hilo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *