Thursday , 28 March 2024
Home Gazeti Habari Chongolo awapa ujumbe viongozi wote wa CCM
HabariHabari za Siasa

Chongolo awapa ujumbe viongozi wote wa CCM

Spread the love

KATIBU Mkuu wa chama tawala nchini Tanzania- Chama Cha Mapinduzi (CCM), Daniel Chongoloamewataka viongozi ngazi zote nchini kuhakikisha wanashiriki vikao vya mashina ili kuendelea kukiimarisha chama hicho kwani msingi wa uimara wa CCM ni ngazi hizo. Anaripoti Mwandishi Wetu, Shinyanga…(endelea).

Aidha, mtendaji mkuu huyo wa chama tawala amezielekeza halmashauri kuacha kugawanya fedha wanazopata katika miradi mingi hivyo kushindwa kuikamilisha au kukamilika kwa kusuasa suasa.

Chongolo ameyasema hayo leo Jumatatu tarehe 30 Mei 2022 mkoani Shinyanga katika shina namba 6 wilayani Kishapu kwenye ziara yenye lengo la kukagua na kuhamasisha uhai wa chama pamoja na kukagua utekelezaji wa miradi ya maendeleo.

“Niwaombe viongozi wenzangu ngazi zote kuanzia tawi, Kata, Wilaya, Mkoa na Taifa tushuke chini kushiriki vikao vya balozi ngazi za mashina, kwani mshina ndio uimara wa chama chetu,” amesema.

Kutokana na changamoto za baadhi ya miradi kuchelewa kukamilika kwa uhaba wa fedha, Chongolo amezielekeza halmashauri kuacha kugawanya fedha katika miradi mingi hivyo kushindwa kuikamilisha na badala yake, amezitaka zielekeze fedha katika miradi michache ya kipaumbele itakayotekelezwa kwa ukamilifu.

Katika maelekezo yake wakati akikagua mradi wa daraja la Ipeja-Itilima wilayani Kishapu, Chongolo amesema ni vema kwa halmashauri kuelekeza fedha katika miradi michache itakayokamilika.

“Sio mnapewa bilioni moja mnapeleka kwenye miradi 40, ambayo haikamiliki, hizo zama zimepita tunataka fedha zielekezwe kwenye mradi unaokwenda kukamilika kwa asilimia 100,” amesema

“Na sio fedha zitolewe kidogo kidogo zikafanye kazi kidogokidogo tija yake haionekani, hayo ndiyo mambo tunayotaka,” amesisitiza.

Hata hivyo, amepongeza hatua ya kukamilika kwa mradi wa daraja hilo, lililogharimu Sh486.4 milioni badala ya Sh500 milioni zilizotengwa.

Katika hatua nyingine, Chongolo aliahidi kushinikiza upatikanaji wa fedha kutoka mfuko wa dharura kugharimia ujenzi wa mradi wa barabara ya Kolandoto-Meatu yenye urefu wa kilometa 53.

Barabara hiyo inayounganisha mikoa ya Shinyanga, Simiyu, Singida na Manyara, alisema itajengwa kwa kiwango cha lami.

Kwa upande wake, Kaimu Meneja wa Wakala wa Barabara Tanzania (Tanroads) Mkoa wa Shinyanga, Ferdnand Mdoe, amesema makadirio ya ujenzi wa barabara hiyo kipande cha mkoa huo pekee ni Sh70 bilioni.

Amesema barabara hiyo inaanzia Kolandoto inapita Lalago, Sibiti, Haidom, Mbulu hadi Karatu ikihusisha Mikoa ya Shinyanga, Simiyu, Singida, Manyara na Arusha.

Amesema tayari upembuzi yakinifu na usanifu ulishakamilika na Sh2 bilioni zimetengwa kugharimia ujenzi wake na hivyo zitakazopelekwa na C hongolo zitaongeza katika kiasi kilichopo.

“Kilio kikubwa cha wananchi ni ujenzi wa kilomita 35 za mwanzo kutoka Kolandoto hadi Munze. Lakini mipango yetu kwa sasa ni kuendelea kuikarabati barabara kwa kiwango cha changarawe,” amesema.

Amesema Serikali hugharimika takribani 600 milioni kila mwaka kwa ajili ya matengenezo hayo na kwamba ndiyo inayotumika kusafirishia Pamba na mifugo.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Kapinga kuongoza usambazaji wa mitungi ya gesi 10,000 ya Taifa Gas

Spread the loveNaibu Waziri wa Nishati, Judith Kapinga ameahidi kuongoza kwa ufanisi...

Habari za SiasaTangulizi

Deni la Serikali laongezeka kwa trilioni 11

Spread the loveDENI la Serikali imeongezeka kwa takribani Sh. 11 trilioni sawa...

Habari za SiasaKimataifa

Mwanaye rais jela miaka miaka 6 kwa dawa za kulevya

Spread the loveMwanawe rais wa zamani wa Guinea-Bissau amehukumiwa kifungo cha miaka...

Habari za SiasaTangulizi

Mapya yaibuka wamasai waliohamishwa Ngorongoro kwenda Msomera

Spread the loveMAPYA yameibuka kuhusu zoezi la Serikali kuwahamisha kwa hiari wamasai...

error: Content is protected !!