Wednesday , 8 May 2024
Home Kitengo Maisha Elimu DIT yatakiwa kujipanga kufunga mfumo wa gesi magari ya serikali, mwendokasi
Elimu

DIT yatakiwa kujipanga kufunga mfumo wa gesi magari ya serikali, mwendokasi

Spread the love

 

NAIBU Katibu Mkuu Wizara ya Nishati nchini Tanzania, Kheri Abdul Mahimbali leo ametembelea Taasisi ya Teknolojia Dar es Salaam (DIT) na kupata fursa ya kuona ufungaji mfumo wa Gesi Asilia kwenye magari unaufanywa na wataalam wa DIT. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Mahimbila amesema lengo la ziara hiyo aliyoifanya jana Ijumaa tarehe 6 Mei 2022 ni kujifunza na kutangaza, kuelimisha na kuhamasisha Watanzania umuhimu wa kutumia gesi asilia.

Alitoa rai kwa DIT kutangaza na kuelimisha umma ili waione fursa hiyo na kuichangamkia.

“Serikali tunalisimamia jambo hili na tumeanza kuhamasisha magari ya serikali kuwekewa mfumo huu ili kupunguza matumizi ya dizeli na petroli,” alisema Mahimbila.

Hata hivyo, aliitaka DIT kujipanga kubadilisha mfumo wa dizeli pia kwa kuwa kwa sasa kazi kubwa inafanyika kwa magari ya petroli pekee.

Alisema magari ya mwendo kasi nayo yataingia katika mpango huo wa kutumia gesi siku za karibuni.

Katika ziara hii alitembelea karakana ya kuweka Mfumo wa Gesi kwenye magari (CNG) iliyopo DIT kuona uwekaji wa mfumo huo, ambapo kwasasa magari 149 ya Shirika la Maendeleo la Petroli (TPDC) unaendelea kwa makubalino yaliyoridhiwa na Kampuni Tanzu ya DIT (DIT Co. Ltd) na TPDC.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

ElimuHabari za Siasa

Serikali kuongeza wanufaika mikopo ya elimu ya juu

Spread the loveSERIKALI imesema itaongeza idadi ya wanufaika wa mikopo ya elimu...

ElimuHabari za Siasa

Serikali kufumua mitaala ya vyuo vikuu, ufundi stadi

Spread the loveSERIKALI inakusudia kufanya mapitio katika mitaala na programu za vyuo...

ElimuHabari Mchanganyiko

Chongolo aagiza TAKUKURU kuchunguza ujenzi wa bweni

Spread the loveMkuu wa Mkoa wa Songwe, Daniel Chongolo amemuagiza Kamanda wa...

ElimuHabari Mchanganyiko

Ugawaji taulo za kike watajwa kutokomeza utoro shuleni

Spread the loveBAADHI ya wanafunzi na walimu wa shule za sekondari mkoani...

error: Content is protected !!