Monday , 6 May 2024
Home Habari Mchanganyiko TUCTA wapendekeza kima cha chini cha mishahara kuwa Sh milioni 1
Habari MchanganyikoTangulizi

TUCTA wapendekeza kima cha chini cha mishahara kuwa Sh milioni 1

Spread the love

SHIRIKISHO la Vyama vya Wafanyakazi Nchini (TUCTA) limesema baada ya kufanya tafiti linapendekeza kiwango cha chini cha kumwezesha mfanyakazi kuishi kiwe Sh milioni 1,010,000 kwa mwezi. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea).

Kauli hiyo imetolewa leo tarehe 1 Mei, 2022 na Katibu Mkuu wa Tucta, Henry Mkunda wakati akizungumza katika sherehe za siku ya wafanyakazi duniani inayofanyika katika uwanja wa Jamuhuri jijini Dodoma.

Amesema TUCTA inatambua changamoto zilizotokana na UVIKO – 19 dunia pia vita ya Urusi na Ukraine vilivyopelekea kuyumba kwa uchumi duniani, lakini bado TUCTA wanaiomba serikali iweke kiwango halisi kitaifa cha malipo ya kima cha chini cha mishahara kitakachowezesha pamoja na wategemezi wao kuishi.

“Aidha, tunakumbuka pia ahadi yako ya kuboresha mishahara kwa wafanyakazi katika mwaka huu wa 2022,” amesema.

Katibu Mkuu huyo pia ametaja sababu za kuchagua kauli mbiu ya sherehe hizo za Mei Mosi ambayo ni “Mishahara na maslahi bora kwa wafanyakazi ndio kilio chetu” kazi iendelee!,”

Amesema sababu zilizowasukuma kupitisha kauli mbiu hiyo kwa mwaka huu ni kutokana na ukweli kwamba wafanyakazi hawajaongezwa mishahara kwa miaka tisa kwa sekta binafsi na miaka saba kwa sekta ya umma.

Amemsema hali hiyo imesababisha kupungua kwa ari ya kufanya kazi hivyo kupunguza ufanisi uwajibikaji na tija mahala pa kazi.

Amesema tafiti zinaonesha kwamba, mishahara na masilahi kwa wafanyakazi humwezesha kufanya kazi kwa ubora, ufanisi na weledi.

“Aidha, pamoja na yote hayo ni wazi kuwa gharama za maisha zimezidi kupanda ilihali stahiki na ujira wa wafanyakazi zimeendelea kuwa duni.

“Kima cha chini cha mishahara kwa watumishi wa sekta zote kimeendelea kuwa duni ikilinganishwa na hali halisi ya kupanda kwa maisha.

“Mathalani katika sekta binafsi kima cha chini cha mshahara ni kati ya Sh 40,000 na 60,000 kwa mtumishi wa nyumbani, kwa watumishi wa mashambani na viwanda kima cha chini ni Sh 100,000.

Viwango hivi vilitangazwa Gazeti la serikali kupitia tangazo la serikali namba 196 la mwaka 2013.

“Kwa upande wa wafanyakazi kenye sekta ya umma, kima cha chini ni Sh 300,000 kiwango kilichotangazwa mwaka 2015,” amesema.

Amesema kutokana na hali hiyo TUCTA ilifanya utafiti na mwaka 2006 na kuwasilisha serikali mapendekezo ya kima cha chini cha mshahara kinachomwezesha kumudu mahitaji muhiumu kama chakula, kodi ya pango, matibabu, kusomesha watoto, mavazi, usafiri wa kwenda na kurudi kazini na kubaini kuwa kiwango cha Sh 315,000 kwa wakati huo ingetosha kumudu gharama za maisha.

Aidha, amesema TUCTA ilifanya utafiti mwingine pia 2014 na kubaini kuwa malipo ya kima cha chini cha mshahara ya Sh 720,000 kwa wakati huo kingemwezesha mfanyakazi kumudu gharama za maisha.

Hata hivyo, pamoja na mapendekezo hayo ya TUCTA juu ya kiwango cha kima cha chini cha kila mwaka, viwango hivyo havijakubaliwa na serikali.

“Kutokubaliwa kwa viwango hivyo kunawaathiri sana wafanyakazi na familia zao kutokana na kupanda kwa gharama za maisha, hali hii imewafanya wafanyakazi kuishi maisha ya chini ya mstari wa masikini,” amesema.

Hata hivyo, akihutubia katika maadhimisho hayo, Rais Samia Suluhu Hassan amejibu ombi hilo na kuwadhibitishia kuwa mishahara itaongezwa lakini si kwa kiwango hicho.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Mahakama yatoa uamuzi zuio dhidi ya Club House

Spread the loveMAHAKAMA Kuu ya Tanzania, Masjala Kuu jijini Dar es Salaam,...

Habari Mchanganyiko

GGML, OSHA yawanoa bodaboda 200 Arusha

Spread the loveZAIDI ya madereva bodaboda 200 wa jiji la Arusha wamepatiwa...

Habari za SiasaTangulizi

Jacob, Malisa wapandishwa kizimbani kwa mashtaka ya uongo mitandaoni

Spread the loveMKURUGENZI wa Shirika la Haki, Godlisten Malisa na mwanachama wa...

BiasharaHabari Mchanganyiko

Serikali kuwakopesha wajasiriamali 18.5bn/- kupitia NMB

Spread the loveSerikali imetenga kiasi cha Sh 18.5 bilioni kwa ajili ya...

error: Content is protected !!