Saturday , 20 April 2024
Home Kitengo Biashara Benki ya NBC yaing’arisha Kariakoo Derby
Biashara

Benki ya NBC yaing’arisha Kariakoo Derby

Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Taifa ya Biashara (NBC) ambae ni mdhamini Mkuu wa Ligi Kuu ya Soka ya Tanzania Bara, NBC Premiere League, Theobald Sabi (kushoto) akikabidhi hundi yenye thamani ya sh milioni moja kwa mchezaji wa klabu ya Simba, Clatous Chama aliyetangazwa mchezi bora wa ligi hiyo kwa mwezi Machi wakati wa mechi kati ya Simba na Yanga iliyofanyika kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam jana. Anayeshuhudia ni Meneja Uhusiano wa benki hiyo, Godwin Semunyu (Kulia)
Spread the love

BENKI ya Taifa ya Biashara (NBC) ambayo ni mdhamini Mkuu wa Ligi Kuu ya Soka ya Tanzania Bara, (NBC Premiere League) jana tarehe 30 Aprili, 2022 iliipamba mechi ya watani wa jadi katika soka la Tanzania kati ya Yanga na Simba kwa kuandaa matukio kadhaa. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea).

Matukio hayo yaliwalenga wapenzi wa mchezo huo pamoja na wateja wa benki hiyo ikiwemo kukabidhi tuzo na zawadi kwa mchezaji bora na kocha bora wa mwezi Machi katika ligi hiyo.

Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Taifa ya Biashara (NBC) ambaye ni mdhamini Mkuu wa Ligi Kuu ya Soka ya Tanzania Bara, NBC Premiere League, Theobald Sabi (kushoto) akikabidhi tuzo kwa mchezaji wa klabu ya Simba, Clatous Chama aliyetangazwa mchezi bora wa ligi hiyo kwa mwezi Machi wakati wa mechi kati ya Simba na Yanga iliyofanyika kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam jana.

Shughuli zote hizo ziliongozwa na maofisa waandamizi wa benki hiyo wakiongozwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki hiyo, Theobald Sabi ambaye alipata wasaa wa kukabidhi tuzo na zawadi ya fedha kiasi cha sh mil 1, kwa mchezaji wa klabu ya Simba Clatous Chama alietangazwa mchezaji bora wa ligi hiyo kwa mwezi Machi sambamba na Kocha Mkuu wa Klabu hiyo, Pablo Franco ambaye pia alitangazwa kocha kwa mwezi huo na hivyo kuzawadiwa tuzo pamoja na fedha kiasi cha sh milioni moja kutoka kwa mdhamini huyo.

Tukio hilo lililoshuhudiwa na maelfu ya mashabiki waliojitokeza kutazama mechi hiyo katika Uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam, lilitanguliwa na matukio mengine ikiwemo mapokezi ya wateja wa benki hiyo kutoka mikoa mbalimbali hapa nchini waliobahatika washindi katika Droo ya Jaza Kibubu Na NBC.

Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Taifa ya Biashara (NBC) ambae ni mdhamini Mkuu wa Ligi Kuu ya Soka ya Tanzania Bara, NBC Premiere League, Theobald Sabi (kushoto) akikabidhi hundi yenye thamani ya sh mil 1 kwa kocha wa klabu ya Simba, Pablo Franco alietangazwa kocha bora wa ligi hiyo kwa mwezi Machi wakati wa mechi kati ya Simba na Yanga iliyofanyika kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam jana.

Washindi hao walipata fursa ya kushuhudia mechi hiyo wakiwa wamelipiwa gharama zote ikiwemo za usafiri, malazi sambamba na kupatikiwa tiketi za VIP kwa ajili ya kushuhudia mtanange huo uliomalizika kwa sare ya bila kufungana.

Pamoja na washindi hao benki hiyo pia iliandaa mwaliko rasmi kwa ajili ya wateja wake mashuhuri wakiwemo viongozi waandamizi kutoka mashirika na taasisi mbalimbali pamoja na wadau wengine wa benki hiyo waliopata wasaa kupata chakula cha mchana pamoja na viongozi wa benki ya NBC kisha kwa pamoja walielekea Uwanja wa Taifa kushudia mechi hiyo wakiwa katika msafara maalum.

Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Taifa ya Biashara (NBC) ambae ni mdhamini Mkuu wa Ligi Kuu ya Soka ya Tanzania Bara, NBC Premiere League, Theobald Sabi (Kushoto) akikabidhi tuzo kwa kocha wa klabu ya Simba Pablo Franco alietangazwa kocha bora wa ligi hiyo kwa mwezi Machi wakati wa mechi kati ya Simba na Yanga iliyofanyika kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam jana.

Aidha, mashabiki waliojitokeza kutazama mechi hiyo walipata fursa ya kupata huduma mbalimbali za kifedha kutoka benki ya NBC kupitia maofisa wake mbalimbali waliokuwa wakitoa huduma hizo kwenye viunga vya vya uwanja huo, hatua iliyotoa fursa kwa mamia ya mashabiki hao kujiunga na huduma za benki hiyo ikiwemo kufungua akaunti mbalimbali pamoja na kufanya mihamala ya kifedha wakiwa maeneo hayo.

Mkurugenzi wa Kitengo cha Biashara kwa wateja wadogo na wa kati kutoka Benki ya NBC, Elvis Ndunguru (kushoto) akiwaongoza wadau mbalimbali wa benki hiyo wakiwemo viongozi waandamizi kutoka mashirika na taasisi mbalimbali pamoja na wadau wengine wa benki hiyo kupata chakula cha mchana kabla ya kuelekea kutazama mechi kati ya Simba na Yanga.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

BiasharaHabari Mchanganyiko

Wauguzi, madaktari 1000 kugawiwa mitungi ya Oryx Gas

Spread the loveKAMPUNI ya Oryx Gas na Taasisi ya Doris Mollel Foundation...

BiasharaHabari za Siasa

Mavunde aagiza Perseus kuharakisha fidia Sengerema

Spread the loveWaziri wa Madini, Anthony Mavunde ameipongeza Kampuni ya Perseus kwa...

Biashara

Black Gold kasino mgodi wa madini Meridianbet 

Spread the love  Dhahabu ni moja kati ya utajiri wenye thamani kubwa...

BiasharaHabari Mchanganyiko

NMB Pesa Akaunti yawavutia wakaguzi wa ndani Afrika

Spread the loveUbunifu wa bidhaa bora wa Benki ya NMB pamoja na...

error: Content is protected !!