Wednesday , 8 May 2024
Home Kitengo Habari Kimataifa Msako waendelea Kenya mauaji mwanariadha wa kike
Kimataifa

Msako waendelea Kenya mauaji mwanariadha wa kike

Spread the love

 

MWANARIADHA wakike amepatikana ameuawa huko Iten mji wa Kenya ,ambapo mwanariadha wa Olimpiki Agnes Tirop aliuawa miezi sita iliyopita polisi wameripoti. Anaripoti Rhoda Kanuti kwa msaada wa Mashirika ya Kimataifa … (endelea).

Mwanariadha huyo Damaris Muthee Mutua ambaye ni mzaliwa nchini Kenya lakini alikuwa na uraia wa Bahrain,mwenye umri wa miaka 28 , amepatikana ameuawa huko Iten mji wa Kenya ambapo mwanariadha mwingine alikutwa ameuawa mwezi oktoba mwaka jana 2021.

Maafisa wanasema kuwa mwanariadha huyo aliuawa kwa kudungwa kisu.

Serikali inamsaka mpenzi wa mwanariadha huyo wa Ethiopia ambaye polisi wanasema kuwa ni mshukiwa mkuu wa tukio hilo.

Aidha Iten ni kambi ya mafunzo kwa wakimbiaji wa masafa marefu.

Hata hivyo mumewe bado yuko kizuizini na anakanusha mashitka hayo kuhusika na mauaji .

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaKimataifa

Israel yatia shubiri Gaza wakisherehekea Hamas kusitisha mapigano

Spread the loveWAKATI kundi la Hamas huko Gaza likitangaza kuridhia pendekezo lao...

KimataifaMakala & Uchambuzi

Mbivu, mbichi urais wa Ramaphosa mwezi huu

Spread the loveMWISHONI mwa mwezi huu, raia wa Afrika Kusini watapiga kura...

Habari za SiasaKimataifa

Mwanamke Rwanda ataka kupambana tena na Kagame

Spread the loveKIONGOZI wa kihistoria wa upinzani nchini Rwanda, Victoire Ingabire Umuhoza,...

Habari MchanganyikoKimataifa

Ruto amteua Kahariri kuwa mkuu wa majeshi

Spread the loveRAIS wa Kenya, William Ruto, amemteua Jenerali Charles Muriu Kahariri,...

error: Content is protected !!