Thursday , 2 May 2024
Home Kitengo Maisha Elimu Idadi uandikishaji wanafunzi MEMKWA yapungua
Elimu

Idadi uandikishaji wanafunzi MEMKWA yapungua

Waziri wa Ofisi ya Rais-TAMISEMI, Innocent Bashungwa
Spread the love

 

SERIKALI imesema uandikishaji wa wanafunzi wa Mpango wa Elimu ya Msingi kwa Walioikosa (MEMKWA) umepungua kutoka 50,192 mwaka 2021 hadi 12,421 mwaka 2022. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dodoma … (endelea).

Hayo yamebainishwa leo Alhamisi tarehe 14 Aprili 2022 bungeni jijini Dodoma na Waziri wa Ofisi ya Rais-TAMISEMI, Innocent Bashungwa wakati akiwasilisha makadirio ya mapato ya mwaka 2022/23 ya wizara yake.

“Hadi mwezi Februari 2022 yanaonesha kupungua ambapo wanafunzi 12,421 wakiwemo wavulana 6,880 na wasichana 5,541 wameandikishwa.

“Idadi hiyo imepungua kwa asilimia 75.25 ikilinganishwa na wanafunzi 50,192 wakiwemo wavulana 27, 819 na wasichana 22,373 walioandikishwa mwaka 2021,” amesema Bashungwa.

Bashungwa alitaja sababu za kupungua kwa idadi hiyo kuwa ni mafanikio ya utekelezaji wa Mpango wa Elimumsingi Bila Malipo.

Amesema kuanzia mwaka 2015 hadi Februari, 2022 mpango umewezesha wanafunzi wenye umri wa kwenda shule kuandikishwa kutokana na kuondolewa kwa ada na michango mbalimbali ambayo ilikuwa ni vikwazo

Ametaja sababu nyingine kuwa ni kutokana na kusogeza huduma za Elimumsingi karibu na wanafunzi kwa kujenga na kuboresha Vituo shikizi vilivyowapunguzia wanafunzi kutembea umbali mrefu kufuata huduma ya elimu.

“Hii inaashiria kwamba wanafunzi waliokuwa wanakosa nafasi ya elimu katika mfumo rasmi sasa wanapata fursa hiyo. Aidha, uandikishaji wa watoto wenye umri wa kwenda shule unafanyika kwa wakati,” amesema.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

ElimuHabari Mchanganyiko

Chongolo aagiza TAKUKURU kuchunguza ujenzi wa bweni

Spread the loveMkuu wa Mkoa wa Songwe, Daniel Chongolo amemuagiza Kamanda wa...

ElimuHabari Mchanganyiko

Ugawaji taulo za kike watajwa kutokomeza utoro shuleni

Spread the loveBAADHI ya wanafunzi na walimu wa shule za sekondari mkoani...

ElimuHabari za Siasa

MbungeCCM ataka kasi uzalishaji walimu ipunguzwe akidai hakuna ajira

Spread the love  MBUNGE wa Mlalo (CCM), Rashid Shangazi, ameishauri Serikali ipunguze...

ElimuHabari za Siasa

Walimu 52,551 kupandishwa madaraja mwaka huu

Spread the loveNaibu Waziri wa nchi, Ofisi ya Rais (Utumishi na Utawala...

error: Content is protected !!