August 15, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Shule za msingi zakabiliwa upungufu walimu 100,958

Waziri wa Ofisi ya Rais-TAMISEMI, Innocent Bashungwa

Spread the love

 

SHULE za Msingi nchini zinakabiliwa na upungufu wa walimu 100,958 kwa kuangalia uwiano wa mwalimu mmoja kwa wanafunzi 60. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dodoma … (endelea).

Hayo yamebainishwa leo Alhamisi tarehe 14 Aprili katika hotuba ya Ofisi ya Rais-TAMISEMI iliyowasilishwa bungeni na Waziri Innocent Bashungwa.

Katika hotuba hiyo Bashungwa amesema takwimu zilizopo zinaonesha kuwa kuna jumla ya Shule za Msingi 17,034 zenye jumla ya wanafunzi 12,033,594 wakiwemo wanafunzi wenye mahitaji maalum 60,825.

Amesema hadi Machi, 2022 mahitaji ya walimu katika Shule za Msingi ni 274,549 kwa kutumia uwiano wa mwalimu mmoja kwa wanafunzi 60 huku walimu waliopo ni 173,591.

“Upungufu ni walimu 100,958 sawa na asimilia 36.77 ya mahitaji,” amesema Bashungwa.

Aidha, amesema mahitaji ya walimu kwa wanafunzi wenye mahitaji maalum kwa Shule za Msingi ni ni walimu 3,631, waliopo ni 1,517 na upungufu ni walimu 2,143 sawa na asilimia 59.02 ya mahitaji.

error: Content is protected !!