Thursday , 2 May 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Mkituletea mazito hatutayatekeleza: Samia aionya TCD
Habari za SiasaTangulizi

Mkituletea mazito hatutayatekeleza: Samia aionya TCD

Rais Samia Suluhu Hassan
Spread the love

RAIS Samia Suluhu Hassan amekitaka kituo cha Demokrasia Tanzania (TCD) kujadili na kutoa kwa Serikali mapendekezo yanayotekelezeka. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dodoma … (endelea).

Ameyasema hayo leo Jumanne tarehe 5 Aprili 2022 awakati akifungua mktano wa kitaifa wa maridhiano, haki na amani ulioandaliwa na TCD.

“Mategemeo yetu kikosi kazi kipo kitakuja na yale mtakayojadili na matumaini yangu mtatuletea yale yanayotekelezeka, mkitupa mazito hatutayatekeleza na itabidi mnune na wanasema ‘gabage in, gabage out’ (ukiweka taka zitazoka taka) kwahiyo mkitutilia ‘gabage’ hapo zitatoka ivo ivo ‘gabage’ lakini mkiweka mazuri basi tutatekeleza vizuri,” amesema Rais Samia.

Mkuu huyo wa nchi ameitaka TCD kuzingatia hali halisi na mazingira ya Tanzania katika majadiliano yao.

“Nawaomba tuzungumzeni kwa mazingira yetu, hali yetu ya siasa, hali yetu ya uchumi na mazingira yetu ya kitanzania. Kama mimi nimetoa roho rahim kwenu nanyi rudisheni roho rahim.”

Amesema fursa ya kukutanana ni nafasi hadhimu ya kujadiliana na kufikia mwafaka wa kitaifa kama Watanzania.

“Niwaombe tutakayoyazungumza hapa tutazungumza kama watanzania. Tunapozungumza mardihiano tunazungumza vipi tunazungumza yapi tutakwenda mpaka wapi. tunaingia kwenye haki zetu kama watanzania ni zipi kama vyama vya siasa ni zipi na pale tulipofungua haki tuzungumze tutakavyoifungua, na tukitoka hapo sasa tunakwedna kudunmisha amani ya nchi yetu,” amesema na kusisitiza;

“Hakuna atakayetusaidia hapo , tutasaidiwa kukusanyika hapa, tutasaidiwa maposhona usfiri lakini haya matatu ni sisi…unapozungumza haki ujue haki yako inapoishia ya mwingine inaanza usije kujadili yako ukataka kubinya ya mwenzako, ” amesema.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Spika Tulia aibana Serikali mafao ya wastaafu Jumuiya ya Afrika Mashariki

Spread the loveSPIKA wa Bunge, Dk. Tulia Ackson ameitaka Serikali kufanya tathimini...

Habari za Siasa

Serikali yawapa maagizo Ma-RC udhibiti magonjwa yasiyoambukiza

Spread the loveWAKUU wa mikoa nchini wametakiwa kuandaa utaratibu wa kuwawezesha wananchi...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Mavunde ataja malengo “Vision 2030”

Spread the loveWAZIRI wa Madini amesema dhana ya “Vision 2030” inakusudia kuiendeleza...

Habari za Siasa

Mavunde aomba bilioni 231.9 bajeti wizara ya madini

Spread the loveWAZIRI wa Madini, Anthony Mavunde leo Jumanne amewasilisha hotuba ya...

error: Content is protected !!